Zúme Training Guidebook

Intensive Course

KIKAO KALI CHA 1

INGIA

(1 min)

Waruhusu washiriki wote na mwezeshaji waingie.

Or six.zume.training/checkin and use code: 1397

OMBA

(5 min)

Anza na maombi. Ufahamu wa kiroho na mabadiliko hayawezekani bila Roho Mtakatifu. Chukua muda kama kikundi kumwalika Yeye ili akuongoze katika kipindi hiki.

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
  • Ufafanuzi rahisi wa Mwanafunzi na Kanisa
  • Kupumua kwa Kiroho ni kusikia na kumtii Mungu
  • Mtumiaji wa Maisha dhidi ya Watumiaji
  • S.O.A.P.S. Kusoma Bibilia
  • Makundi ya Uwajibikaji
  • Jinsi ya kutumia Saa katika maombi
  • Usimamizi wa Jamaa - Orodha ya 100

READ

(5 min)

Mungu Anatumia Watu wa Kawaida

Karibu kwenye mafundisho ya Zume. Zume ni neno la Kigiriki linalomaanisha "chachu."

Yesu anatuambia kwamba Ufalme wa Mungu ni kama mwanamke ambaye alichukua kiasi kidogo cha " Zume" na kukiweka kwenye kiasi kikubwa cha unga uliokandwa.

Alipokuwa akichanganya, chachu ilienea hata unga wote ukachachuka.

Yesu alikuwa anatufundisha kwamba mtu wa kawaida anaweza kutumia kitu kidogo sana na kusababisha kishindo kikubwa sana!

Ndoto yetu ni kufanya yale Yesu alisema -- kuwasaidia watu wa kawaida duniani kote kutumia vifaa vidogo kutoa vishindo vikubwa katika Ufalme wa Mungu!

Maagizo ya Yesu ya mwisho kwa wanafunzi wake yalikuwa rahisi. Alisema -- Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi -enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwa batiza kwa jina la baba, na la Mwana, nala Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Maagizo ya Yesu yalikuwa rahisi -Mkawafanye Wanafunzi

Amri yake jinsi ya kutekeleza hayo ilikuwa rahisi - mkafanye wanafunzi popote muendapo

  • Mkafanye wanafunzi kwa kuwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu
  • Mkawafanye wanafunzi kwa kuwafundisha yote niliyowaamuru

Kwa hivyo ni hatua zipi za kuwafanya wanafunzi?

  • Tunawafanya wanafunzi kila wakati - popote tuendapo na tunapoenda
  • Mtu akifanya uamuzi wa kumfuata Yesu - sharti abatizwe
  • Wanapokua - tufundishe kila mwanafunzi jinsi ya kutii vitu vyote alivyoamuru Yesu.

Kwa vile kitu kimoja alichoamuru ni kufanya wanafunzi, hiyo inamaanisha kila mwanafunzi anayemfuata Yesu anastahili kujifunza jinsi ya kutengeneza wanafunzi pia.

Hao wanafunzi wanastahili kutengeneza wanafunzi. Na hao wanafunzi nao wakatengeneze wanafunzi, pia.

Kuzidisha wanafunzi. Hivyo ndivyo Zume inafanya kazi.

Ni kama chachu - ilijichanganya ndani mwa unga uliokandwa hadi wote ukawa chachu.

Wakati Yesu alipotoa amri hii ya kwenda kuwafanya wanafunzi, alitoa ahadi pia.

Yesu alisema - Nitakuwa nanyi daima. Hata ukamilifu wa dahari.

Kila mfuasi wa Yesu anapaswa kuzingatia ahadi ya kuwa Yesu yu pamoja nasi. Kwa sababu Yeye yuko!

Lakini pia inamaanisha kila mfuasi wa Yesu anapaswa kujitoa kwa ukweli kwamba Yesu anataka kila mmoja wetu atengeneneze wanafunzi. Kwa sababu Yeye alifanya.

Yesu alisema - nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye wanafunzi.

Mamlaka ambayo Yesu hutegemea wakati Anatutuma - ni mamlaka Yake

Yesu anasema hakuna mamlaka iliyo juu kuliko hiyo. Hakuna utamaduni uliyo na mamlaka zaidi.

Hakuna utamaduni uliyo na mamlaka zaidi. Hakuna sheria duniani iliyo na mamlaka zaidi.

Yesu alisema - nendeni mkawafanye wanafunzi.

Na kama Zume - chachu - tutaendelea kuenda na kukua hata kazi yote ikamilike.

JADILI

(10 min)

  1. Ikiwa Yesu alikusudia kila mmoja wa wafuasi Wake kutii Agizo Lake Kuu, kwa nini ni wachache sana wanaofanya wanafunzi?

READ

(5 min)

Wanafunzi na Kanisa

Karibuni tena kwenye mafundisho ya Zume.

Katika kipindi hiki, tutazungumzia kuhusu wanafunzi na kanisa.

Mwanafunzi ni nani?

Na wawezaje kumfanya mmoja? awe mwanafunzi kwa njia gani?

Je, wawezaje kumfundisha mfuasi wa Yesu kutii amri zake zote?

Je, unachukuliaje mtu ambaye aliishi maisha yake kama mtumwa wa ulimwengu na kumwezesha kuwa raia wa ufalme wa Mungu?

Maana ya neno mwanafunzi ni mfuasi.

Kwa hivyo mwanafunzi ni mfuasi wa Mungu.

Yesu alisema - Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.

Kwa hivyo katika ufalme wa Mungu, Yesu ndiye Mfalme wetu.

Sisi ni raia wake, kwa mapenzi yake.
Wapenzi wake, makusudi, malengo yake, vipaumbele na maadili ni vya juu na bora zaidi.

Neno lake ni sheria. Kwa hivyo sheria ya ufalme ni nini? Je! Yesu anawaambia watu wake wakafanye nini?

Yesu alisema - Mpende Bwana Mungu kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.
Yesu alisema - Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.

Yesu alisema kwamba amri za Mungu ktika Agano la Kale - sheria zote na manabii - zinaweza kufupishwa katika mambo haya mawili - mpende Mungu na Uwapende Watu

Yesu alisema - Fanya wanafunzi

Yesu alisema - Wafundishe kutii yote niliyoamuru.

Kwa kuwa kufanya wanafunzi inajumuisha kuwafundisha yote Yesu aliyoamuru - Agano Jipya inaweza kufupishwa kwa jambo moja - Wafanye Wanafunzi

Mwanafunzi ni mfuasi wa Yesu anayempenda Mungu, anapenda watu na huwafanya wanafunzi

Basi kanisa ni nini?


Huenda huwa unafikiria kanisa ni jengo - mahali unapoenda.

Lakini Neno la Mungu linazungumzia kanisa kama mkusanyiko - watu ambao wewe umo miongoni mwao.

Neno "kanisa" linatumiwa katika Biblia kwa njia tatu tofauti:

  • kanisa la ulimwengu wote - watu wote ambao walikuwa, ambao wapo na ambao daima watakuwa wafuasi wa Yesu
  • kanisa la jiji au la kanda - watu wote wanaomfuata Yesu na wanaishi humo au karibu na eneo fulani la ulimwengu
  • kanisa la nyumbani - watu wote wanaomfuata Yesu na hukutana pahali mmoja ama watu wengi wanapoishi.

Familia ya kiroho - wafuasi wa Yesu wanaompenda Mungu, wanawapenda watu na kuwafanya wanafunzi ambao hukutana kwenye mitaa yao ndio aina ya mwisho ya kikundi hiki cha kanisa - kanisa la nyumbani au kanisa vivi hivi.

Wakati makundi ya makanisa haya yanapokutana kufanya kitu kikubwa, kwapamoja, wanaweza kutengeza kanisa la jiji au kikanda.
Makanisa hayo yote vivi hivi yameunganishwa katika mikoa na kuenea katika historia kufanya kanisa zima.

HILO NI KANISA NA HERUFI "K" KUBWA
Makanisa yakawaida ni familia za kiroho na Yesu kama kiungo cha kati na mfalme wao.

Makanisa ya kawaida ni familia za kiroho za wanaompenda Mungu, wanawapenda wengine na wanawafanya wanafunzi ambao wanajizidisha.

Makanisa mengine yana majengo na orodha na matumizi na wafanyi kazi. Lakini makanisa yakawaida hayana haja na vitu hivi ili wampende Mungu, wapende wengine na kuwafanya wanafunzi ambao wanajizidisha idadi.

Na kwa kuwa chochote cha ziada hulifanya kanisa kuwa na ugumu kujizidisha, mafundisho yetu huacha vitu kama majengo na orodha na matumizi na wafanya kazikwa kanisa la jiji la kanda lililojengwa kutokana na uzidishaji wa makanisa yakawaida.

Kumbuka kwamba "zume" inamaanisha "chachu" -- kiumbe ambacho kinazalisha haraka haraka.

Kupitia mafundisho ya Zume - tutakuwa kama ile chachu - vivi hivi na kujizidisha.
Lakini kabla tuanze kujizidisha -tuhakikishe kwamba tunajua kile Mungu anataka kizalishwe.
Kwa sababu kuzidisha kunaweza kuwa kuzuri - lakini sio kila mara.

Saratani hujizidisha. Na inaua.

Tunawezaje kuzalisha uhai na sio kifo? Tunawezaje kuhakikisha kwamba sisi ni wanafunzi wanaoweza kuzalisha?

JADILI

(10 min)

  1. Unapofikiria kuhusu kanisa, kitu gani huja mawazoni?
  2. Kuna tofauti gani kati ya picha hiyo na kile kinachofafanuliwa kwenye video kama "Kanisa Rahisi"?
  3. Unafikiri ni gani ingekuwa rahisi kuzidisha na kwa nini?

READ

(5 min)

Kumsikia na Kumtii Mungu

Karibu tena kwenye mafundisho ya Zume.

Katika kipindi hiki, tutaongea kuhusu kusikia kutoka kwa Mungu na kutii yale tunayosikia.

Kupumua ni maisha.

Tunavuta hewa ndani. Tunatoa hewa nje, ni uhai.

Kupumua ni muhimu katika Ufalme wa Mungu.

Kwa kweli, Mungu anaita Roho Wake - "pumzi"

Katika Ufalme, tunapumua ndani tunaposikia kutoka kwa Mungu.

Tunapumua wakati tunasikia kutoka kwa Mungu kupitia NENO LAKE - Biblia.

Tunapumua wakati tunaposikia kutoka kwa Mungu kupitia kwa MAOMBI - mazungumzo yetu naye.

Tunapumua wakati tunasikia kutoka kwa Mungu kupitia MWILI WAKE - kanisa, wafuasi wengine wa Yesu.

Tunapumua tunaposikia kutoka kwa Mungu kwa njia ya kazi zake - matukio, uzoefu na wakati mwingine hata mateso na kuteseka ambapo anaruhusu watoto wake kupitia.

Katika Ufalme tunapumua NJE tunapotenda kwa ajili ya yale tunasikia kutoka kwa Mungu. Tunapumua NJE wakati TUNATII.

Wakati mwingine kupumua nje kwa KUTII inamaanisha kubadilisha mawazo yetu, maneno yetu au matendo yetu ili kuwaleta pamoja na Yesu na mapenzi Yake.

Wakati mwingine kupumua kwa KUTII kunamaanisha kugawana kile Yesu ameshiriki nasi - kupeana kile alichotupa - ili wengine waweze kubarikiwa kama vile Mungu anavyotubariki.

Kwa mfuasi wa Yesu - hii kupumua NDANI na kupumua NJE ni muhimu. Ni maisha yetu.

Yesu alisema - Mwana hawezi kufanya kitu peke yake. Anafanya tu yale anayoyaona Baba akifanya. Chochote Baba anachofanya, Mwana pia hufanya.

Yesu alisema - Sineni kwa mamlaka yangu mwenyewe. Baba aliyenituma ameniamrisha cha kusema na jinsi ya kusema.

Yesu alisema kwamba kila neno alilosema na kila kazi aliyotimiza ilitokana na KUSIKIA kutoka kwa Mungu na KUTII yale aliyasikia.

Pumua NDANI - Sikia kutoka kwa Mungu.

Pumua NJE - Tii yale unayosikia na ushiriki na wengine.

Yesu alisema kwamba wafuasi wake pia watasikia kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Roho Mtakatifu wake - Kupumua Kwake - ambayo itapumuliwa ndani ya kila mmoja wetu anayemfuata.

Yesu alisema - Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha vitu vyote na kuwakumbusheni kila kitu nilichowaambia.

Kupumua NDANI- Sikia kutoka kwa Mungu.

Pumua NJE- Tii yale unayoyasikia na uishiriki na wengine.

Yesu alikuwa anatuonyesha jinsi ya kuishi.

Kwa hivyo tunaisikiaje sauti ya Mungu? Tunajuaje nini cha kutii?

Yesu alijiita mwenyewe "Mchungaji Mzuri". Yesu aliwaita wafuasi "kondoo"wake.

Yesu akasema - Kondoo wangu husikia sauti Yangu, na ninawajua, na wananifuata.

Yesu alisema - Yeyote aliye wa Mungu husikia kile ambacho Mungu anasema. Sababu hamsikii ni kwamba ninyi si wa Mungu.

Kama wafuasi wa Yesu, tunapaswa kujitolea kusikia sauti Yake.

  • TUNASIKIA sauti yake kwa kuwa kimya.
  • TUNASIKIA sauti yake kwa kumzingatia Yesu.
  • TUNASIKIA sauti yake katika mawazo yetu, maono yetu, hisia zetu na dhana zetu.
  • TUNASIKIA sauti yake tunapoandika na kuhakiki kile tunachosikia.

Si kila sauti, sio kila wazo, sio maono, hisia au dhana ni sauti ya Mungu.

Wakati mwingine ni sauti ya adui

Yesu alisema adui yetu ni mwongo na baba wa uongo. Yesu alisema adui yetu huja kuiba, kuua na kuharibu.

Lakini Mungu anasema kwamba TUTASIKIA kutoka kwake na tutajua ni Yeye wakati anapozungumza

Kwa kujizoeza na maombi, tunaweza kujua sauti ya Mungu vyema. Tunaweza kujifunza kujua kama tunachosikia ni kutoka kwa Mungu au sauti nyingine.

Hapa kuna njia ya kujaribu yale tunayosikia:

  • Wakati Yesu anapoongea - sauti yake itakuwa thabiti Neno lake Lililoandikwa -
  • Biblia - tayari imetueleza. Sauti yake haitakinzana na sauti ilioandikwa.
  • Wakati Yesu anapoongea - sauti yake itaipa mioyo yetu hisia ya tumaini na amani. Sauti yake haitatuacha ama kutuvunja mioyo. Yesu hahukumu. Yesu hurekebisha kwa upendo.
  • Sauti ya Yesu haitaelezea matendo ya mwili - uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu na uchawi, uadai, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, mambo haya sio sauti ya Mungu.
  • Wakati Yesu anapoongea - sauti yake itatuonyesha matunda ya Roho wa Mungu - upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.

Wakati Yesu akisema - Sauti yake hutupa hisia za kujiamini badala ya wasiwasi. Tunapata ndani mwetu ujuzi na amani kwamba kile tunachosikia kinatoka kwa Mungu. Hatuwezi kusikia kila kitu mara moja. Tunaweza kusikia sehemu tu ya kile tunachohitajika kujua. Lakini kile tunasikia itakuwa imara - si ya kuhama hama au kujibadilisha.

Habari njema kwa kila mfuasi wa Yesu ni kwamba tunapopumua NDANI na KUSIKIA kutoka kwa Mungu na tunapopumua NJE na KUTII tunachosikia na kushirikiana na wengine tulichosikia - Mungu ataongea wazi wazi.

Pumzi yake itapumua kupitia sisi hata zaidi.

TUTASIKIA sauti yake wazi zaidi.

TUTAJUA sauti yake na sio nyingine.

TUTAONA kazi ndani yake duniani na kujiunga naye kufanya kazi pamoja

Tunapumua. Tunapumua nje. Uzima.

JADILI

(10 min)

  1. Kwa nini ni muhimu kujifunza na kusikia na kutambua sauti ya Mungu?
  2. Je, kusikia na kumuitikia Bwana ni kama kupumua? Kwa nini au kwa nini sivyo?

READ

(5 min)

S.O.A.P.S. Kusoma Bibilia

Yesu alisema --"mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi…"

Ikiwa kila mfuasi wa Yesu atatii yote ambayo Yesu aliamuru, atahitaji kujua kile Yesu alichoamuru.

Amri Kuu na Agizo Kuu ni muhtasari mkuu wa kile Mungu anatuambia, lakini ili mfuasi akue kikamilifu na awe kile ambacho Mungu alimuumba kuwa, anahitaji kuwa na ufahamu na kutii hata zaidi.

S.O.A.P.S. inamaanisha:

  • Maandiko
  • Uchunguzi
  • Matumizi
  • Sala na
  • Kushiriki

Ni njia rahisi ya kujifunza na kukumbuka mbinu ya kujifunza Biblia yenye ufanisi ambayo mfuasi yeyote wa Yesu anaweza kutumia. Hebu tuangazie kile sehemu kwa undani zaidi.

Unaposoma au kusikiliza Biblia:

  • Maandiko : Andika mstari mmoja au zaidi ambayo ina umuhimu kwako zaidi, leo.
  • Uchunguzi : Andika tena mistari hiyo kutoka kwenye Maandiko hayo kwa maneno yako mwenyewe ili kukusaidia kuelewa vyema zaidi maana iliyoko.
  • Matumizi : Tafakari maana ya kutii amri au dhana hizo katika maisha yako mwenyewe. Utahitaji kufanya nini kwa njia tofauti? Andika mambo hayo.
  • Sala : Andika sala inayomwambia Mungu kile ambacho umekuwa ukisoma katika Neno lake na kile unachoelewa kuhusu kutii amri zake na kutekeleza kile ulichojifunza.
  • Kushiriki : Muulize Mungu anataka ushiriki na nani kile ulichojifunza na jinsi unavyokitumia.

Basi hebu tutumie S.O.A.P.S:

  • Maandiko - Biblia inasema: "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu," asema BWANA. "Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu." Isaya 55:8-9
  • Uchunguzi - Kama mwanadamu, nina mipaka katika kile ninachojua na kile ninachojua jinsi ya kukifanya. Lakini Mungu hana mipaka yoyote. Anaona na anajua kila kitu. Anaweza kufanya lolote lile.
  • Matumizi - Kwa vile Mungu anajua kila kitu na njia zake ndio bora zaidi, nitapata mafanikio zaidi maishani ikiwa nitamfuata badala ya kutegemea njia yangu ya kufanya mambo.
  • Sala - Bwana, sijui jinsi ya kuishi maisha mazuri yanayokupendeza na yanayosaidia wengine. Njia zangu husababisha makosa. Mawazo yangu husababisha maumivu. Naomba unifundishe njia zako na mawazo yako badala yake. Roho wako Mtakatifu aniongoze ninapokufuata.
  • Kushiriki - Nitashiriki mistari hii na matumizi yake na rafiki yangu, Steve, ambaye anapitia wakati mgumu na anahitaji mwongozo kwa ajili ya maamuzi muhimu yanayomkabili.

Kujifunza Biblia Kupitia S.O.A.P.S. Mojawapo ya zana rahisi katika Seti Yetu ya Zana ya Zume.

SHUGHULI

(30 min)

Kichwa: Somo la Biblia la SOAPS

MAUDHUI:

Maandiko

Andika mstari mmoja au zaidi ambayo ni ya maana sana kwako, leo.

Uchunguzi

Andika upya mistari hiyo au mambo muhimu kwa maneno yako mwenyewe ili kuelewa vyema.

Utendaji

Fikiria juu ya nini maana ya kutii amri hizi katika maisha yako mwenyewe.

Maombi

Andika maombi ukimwambia Mungu yale uliyojifunza na jinsi unavyopanga kutii.

Kushikiri

Muulize Mungu ambaye anataka ushiriki naye kuhusu yale uliyojifunza/kutumia.

Hapa kuna mfano wa S.O.A.P.S. kazini:

S - "Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu," asema Bwana. "Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu." Isaya 55:8-9

O - Kama binadamu, nina mipaka katika kile ninachojua na kile ninachojua kufanya. Mungu hana kikomo kwa njia yoyote. Anaona na anajua YOTE. Anaweza CHOCHOTE.

A - Kwa kuwa Mungu anajua kila kitu na njia zake ni bora zaidi, nitakuwa na mafanikio zaidi maishani ikiwa nitamfuata badala ya kutegemea njia yangu mwenyewe ya kufanya mambo.

P - Bwana, sijui jinsi ya kuishi maisha mazuri yanayokupendeza na kusaidia wengine. Njia zangu husababisha makosa. Mawazo yangu husababisha maumivu. Tafadhali nifundishe njia Zako na mawazo Yako, badala yake. Acha Roho wako Mtakatifu aniongoze ninapokufuata Wewe.

S - Nitashiriki mistari hii na matumizi haya na rafiki yangu, Steve, ambaye anapitia wakati mgumu na anahitaji mwelekeo wa maamuzi muhimu anayokabili.

READ

(5 min)

Makundi ya Uwajibikaji

Yesu alisema -"Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi."

Yesu alisimulia hadithi nyingi kuhusu uwajibikaji na alituambia kweli nyingi kuhusu jinsi tutakavyowajibishwa kwa kile tunachofanya na kusema.

Yesu anatuambia mambo haya sasa, ili tuwe tayari kwa ajili ya baadaye. Na kwa vile tutawajibishwa mbele zake siku moja, ni vyema kuwa na tabia ya kuwajibishana sasa.

Makundi ya Uwajibijaki yanaundwa na watu wawili au watatu wa jinsia moja- wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake - wanaokutana mara moja kwa wiki kujadili seti ya maswali yanayosaidia kufichua sehemu ambapo mambo yanaenda vizuri na sehemu zingine zinazohitaji marekebisho.

Kila mfuasi wa Yesu atawajibishwa, hivyo kila mfuasi wa Yesu anapaswa kuwajibika kwa wengine.

Makundi ya Uwajibikaji Zana nyingine rahisi katika Seti Yetu ya Zana ya Zume.

SHUGHULI

(20 min)

Jina: vikundi vya uwajibikaji

Maudhui:

  1. Umemuonaje Mungu akifanya kazi?
  2. Je, umekuwa ushuhuda wiki hii kwa ukuu wa Yesu Kristo kwa maneno na matendo yako yote?
  3. Je, umekabiliwa na nyenzo zinazovutia ngono au kuruhusu akili yako kuwaza mawazo yasiyofaa ya ngono?
  4. Je, umekubali umiliki wa Mungu katika matumizi yako ya pesa?
  5. Umetamani chochote?
  6. Je, umeumiza sifa au hisia za mtu kwa maneno yako?
  7. Je, umekuwa si mwaminifu kwa maneno au matendo au kutia chumvi?
  8. Je, umejihusisha na tabia ya uraibu (au mvivu au isiyo na nidhamu)?
  9. Je, umekuwa mtumwa wa mavazi, marafiki, kazi, au mali?
  10. Umeshindwa kumsamehe mtu?
  11. Je, ni wasiwasi gani au wasiwasi gani unaokumbana nao?
  12. Je, umelalamika au kunung'unika?
  13. Je, umedumisha moyo wa shukrani?
  14. Je, umekuwa ukiheshimu, kuelewa na kuwa mkarimu katika mahusiano yako muhimu?
  15. Je, ni majaribu gani katika mawazo, neno, au matendo ambayo umekumbana nayo na ulijibu vipi?
  16. Je, umechukuaje fursa za kuwatumikia au kuwabariki wengine, hasa waumini?
  17. Je, umeona majibu mahususi kwa maombi?

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
  • Ufafanuzi rahisi wa Mwanafunzi na Kanisa
  • Kupumua kwa Kiroho ni kusikia na kumtii Mungu
  • Mtumiaji wa Maisha dhidi ya Watumiaji
  • S.O.A.P.S. Kusoma Bibilia
  • Makundi ya Uwajibikaji
  • Jinsi ya kutumia Saa katika maombi
  • Usimamizi wa Jamaa - Orodha ya 100

Take a Break

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
  • Ufafanuzi rahisi wa Mwanafunzi na Kanisa
  • Kupumua kwa Kiroho ni kusikia na kumtii Mungu
  • Mtumiaji wa Maisha dhidi ya Watumiaji
  • S.O.A.P.S. Kusoma Bibilia
  • Makundi ya Uwajibikaji
  • Jinsi ya kutumia Saa katika maombi
  • Usimamizi wa Jamaa - Orodha ya 100

READ

(5 min)

Mtayarishaji sio Mtumiaji

Katika kikao hiki, tutazungumzia kuhusu jinsi tunaweza kumsaidia mfuasi wa Yesu kuwa MZALISHAJI katika ufalme wa Mungu badala ya mlaji tu.
Katika mpango wake mkamilifu, Mungu alituumba tuishi katika usawa - KUZAANA na KULA, KUFANYIZA na KUTUMIA, KUMWAGA NJE na KUJAZWA ili tuweze KUMWAGA NJE tena.

Lakini, katika dunia yetu hii, watu wamekataa mpango wake Mungu, na wengi wanatumia nguvu zao kuishi nje ya sehemu ya ulinganisho wa Mungu.

WANAJIFUNZA bali hawashirikiani. WAMEJAZWA bali hawamwagi nje. WANATUMIA bali hawazilishi.

Ikiwa tutawafanya wanafunzi wanaojizidisha, basi tunahitaji kushiriki pamoja nao jinsi wanaweza kuwa wazalishaji na sio watumiaji tu.

Tunaweza kufanya hivyo hapa - Mungu anatumia Neno lililoandikwa - ambalo tunaita maandiko ama Biblia - ili kukua kiroho.

Kila mwanafunzi anahitaji kujiandaa ili akasome, kutafsiri na kutumia maandiko.

Zaidi ya maelfu ya miaka na kwa mikono ya waandishi wengi tofauti, Mungu alinena neno lake ndani ya mioyo ya watu waaminifu ambao walishika na kushirikiana yale waliyoyasikia.

Maandiko yanatufundisha hadithi ya Mungu, mipango yake, moyo wake, njia zake.

Katika kikao cha awali, mlijifunza kuhusu vyombo viwili - masomo ya Biblia ya SOAPS na Kikundi cha Uwajibikaji. Katika kikao kijacho, mtajifunza chombo kimoja kingine - vikundi vya theluthi 3/3.

Vifaa hivi vitatu vinafanya kazi kwa pamoja ili kusaidia wafuasi wapya kujifunza, kutafsiri na kutumia Neno la Mungu lililoandikwa.

Watajifunza sio kuwa tu wasikizaji wa Neno la Mungu bali watendaji na washirika, pia.

Mungu hutumia Neno lake Lililonenwa - ambalo unaweza kutambua kwa njia ya maombi - kutufanya tukue kiroho.

Maombi ni kuzungumza na kumsikiliza Mungu. Maombi hutusaidia kumjua Mungu kwa ukaribu sana na kuelewa moyo wake, mapenzi yake na njia zake.

Maombi hutusaidia katika huduma na kuwatumikia wengine, hutusaidia kufundisha na kushiriki katika njia maalum ambayo husaidia mtu au kikundi kumjua Mungu vizuri.

Vifaa viwili - Kuomba kwa kutembea na kuomba kwa mviringo huwasaidia Wafuasi kuendeleza maombi ya kibinafsi na kujifunza maisha ya maombi ya kibinafsi na kuomba kwa njia ambazo zinahudumia wengine.

Vifaa hivi husaidia kuendeleza tabia ya kuomba bila kukoma na kujifunza kuona dunia kutokana na mtazamo wa kiroho badala ya kutegemea yale tunayoweza kuona tu.

Ikitumika kwa uthabiti, vinasaidia mfuasi wa Yesu, kuongeza uwezo wao wa maombi na kuongeza uwezo wao wa kusikia kutoka kwa Mungu na kushirikiana yale wanayoyasikia.

Mungu hutumia waumini Mwili wake - ambao tunaita Kanisa ama Wafuasi wa Yesu - kutukuza kiroho.

Kama mkusanyiko wa waumini, tumeunganishwa. Neno la Mungu linasema kwamba, katika Yesu - sisi ni sehemu nyingi za mwili mmoja, na tunahusiana. Kwa maneno mengine, hatujaunganishwa tu na Mungu - tumeunganishwa na kila mmoja.

Mungu anasema mjiwasilishe kila mmoja kwa mwenzake. Mungu anasema mkahudumiane.

Kila mmoja wetu ana uwezo tofauti na kila mmoja ana udhaifu. Mungu anatutarajia sisi kuwaruhusu wengine kutusaidia katika udhaifu wetu kwa kutumia uwezo aliyowapa.

Neno la Mungu iinasema Mungu amempa kila mmoja uwezo wa kipekee; zitumie kuwasaidia wengine, kuwapa wengine baraka nyingi za Mungu.

Vifaa vingi kama vile vikundi vya theluthi 3/3, vikundi vya uwajibikaji na Kushauriana Ki rika hutusaidia kuhimizana mmoja kwa mwenzake kiupendo na kazi nzuri sio tu kutusaidia kutii yale Mungu anatueleza kufanya bali inatusaidia kupata njia ya kushiriki na wengine yale tuliyojifunza na wengine.

Mungu pia hutumia udhalimu na mateso - dhabihu na hasara tunayokabiliana nayo kwa ajili ya Yesu - kutufanya tukue kiroho.

Wakati watu wanatuhukumu na kutuumiza kwa sababu tunampenda na kumtii Yesu, ama wakati mambo mabaya yanatutokea pamoja na kwamba tunampenda na kumtii Yesu, Mungu hutumia huo udhalimu na mateso kuboresha tabia zetu kutufanya tuwe kama Yesu.

Yeye hustawisha tabia zetu, hutuimarisha na kutakasa imani yetu, hutuandaa kwa huduma na hutuwezesha kuhudumia wegine ambao wanateseka - wakati wote akijitambulisha waziwazi kwa kila mtu anayetutazama na kuelewa maumivu yetu.

Mungu anatueleza kwamba, kama wafuasi wa Yesu lazima tutarajie mateso.

Yesu alisema - Mungu atawabariki wakati watu wanakutukana, wanakutendea mabaya, na kusema kila aina uongo juu yenu kwa ajili yangu mimi. Kueni na furaha na msisimko! Mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni. Watu waliwafanyia mambo hayo manabii ambao waliishi zamani.

Vifaa kama theluthi 3/3 vya vikundi vya uwajibikaji huwapa wafuasi wa Yesu fursa ya kushiriki udhalimu na mateso wanayopata.

Vikundi hivi vinawapa nafasi ya kufundisha wanafunzi kwamba neno la Mungu linasema tutarajie nyakati ngumu na kuwawezeshea njia ambazo wanaweza kukabiliana nazo kwa kuamini upendo wake Mungu hata wakati mambo yanaenda mrama.

Maandiko. Maombi. Mwili Uzima. Udhalimu na Mateso.

Hivi ndivyo Mungu anatukuza tue bora zaidi kama mwanawe mkamilifu Yesu.

Vifaa vinavyotusaidia sio tu kwa watumiaji wa mambo haya mazuri ambayo Mungu ametupa bali kuwa wazalishaji na washirika pia

JADILI

(10 min)

  1. Katika maeneo manne yaliyo hapo juu (maombi, Neno la Mungu, nk), ni ipi tayari unafanya?
  2. Ni zipi unahisi huna hakika nazo?
  3. Je! Unajisikia tayari kiasi wakati wa kufundisha wengine?

READ

(5 min)

Mfuatano wa Maombi

Yesu mara nyingi alifundisha wafuasi wake kuhusu kusudi, desturi na ahadi za sala.

Yesu alisema -"Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa."

Yesu aliwafundisha wafuasi wake kwamba sala si kwa ajili ya kusifiwa na watu, si kuomba vitu kwa ubinafsi wala si hotuba ndefu isiyo na mwelekeo tunayorudia tena na tena.

Yesu alituonyesha kwamba sala ina nguvu kwa sababu ni mazungumzo ya moja kwa moja yasiyokoma na Baba yetu wa mbinguni atupendaye. Kama mazungumzo yoyote mazuri, sala nzuri inamaanisha kwamba pande zote mbili zinasikiliza -- na kuzungumza. Lakini kuzungumza na Mungu aliyeumba ulimwengu kunaweza kuogopesha. Na kusikia akisema kitu - kwa watu wengi hilo linaweza kushtua sana.

Habari njema ni kwamba kuwa na ustadi katika sala -kuwa na mazungumzo bora na ya kina zaidi na Mungu atupendaye - si tu jambo linalowezakana -bali pia ni jambo analotaka Mungu.

Lakini sala inapohisi kama kujifunza lugha mpya -Utakuwaje na ustadi? Jibu ni rahisi - unajizoeza. Mzunguko wa Sala ni zana rahisi ya kujizoeza sala ambayo unaweza kutumia na kushiriki na mfuasi mwingine.

Kwa hatua 12 tu rahisi - kila moja ikihitaji dakika 5 - Mzunguko wa Sala unakuongoza katika hatua kumi na mbili ambazo kwazo Biblia inatufundisha kuomba. Mwishowe, utakuwa umeomba kwa saa moja. Biblia inatuambia - "Ombeni bila kukoma." Si wengi wetu tunaweza kusema tunafanya hivyo. Lakini katika saa hii moja ya sala - utakuwa umepiga hatua mbele.

Mzunguko wa Sala - Zana nyingine moja zaidi rahisi katika Seti Yetu ya Zana ya Zume.

SHUGHULI

(60 min)

Kichwa: Mzunguko wa Maombi

Maudhui:

Kwa hatua 12 tu rahisi - dakika 5 kila moja - Mzunguko huu wa Maombi unakuongoza kupitia njia 12 ambazo Biblia inatufundisha kuomba. Mwishowe, utakuwa umeomba kwa saa moja.

prayer cycle

SIFA

Anza saa yako ya maombi kwa kumsifu Bwana. Msifu kwa mambo ambayo yako akilini mwako sasa hivi. Msifu kwa jambo moja maalum ambalo amefanya katika maisha yako katika wiki iliyopita. Msifu kwa wema wake kwa familia yako.

SUBIRI

Tumia muda kumngoja Bwana. Nyamaza na umruhusu akuvute tafakari.

UKIRI

Mwombe Roho Mtakatifu akuonyeshe chochote katika maisha yako ambacho kinaweza kuwa hakimpendezi. Mwambie akuonyeshe mitazamo ambayo si sahihi, pamoja na matendo mahususi ambayo bado hujafanya maombi ya kuungama. Sasa ungameni hilo kwa Bwana ili mpate kutakaswa.

SOMA NENO

Tumia muda kusoma katika Zaburi, katika manabii, au vifungu vya maombi vilivyo katika Agano Jipya.

ULIZA

Fanya maombi kwa niaba yako mwenyewe.

MAOMBI

Fanya maombi kwa niaba ya wengine.

OMBA NENO

Omba vifungu maalum. Sala za Kimaandiko na vilevile Zaburi kadhaa hufaa kwa kusudi hilo.

ASANTE

Mshukuru Bwana kwa mambo katika maisha yako, kwa niaba ya familia yako, na kwa niaba ya kanisa lako.

IMBA

Imba nyimbo za sifa au kuabudu au wimbo mwingine au wimbo wa kiroho.

TAFAKARI

Mwombe Bwana aseme nawe. Kuwa na kalamu na karatasi tayari kurekodi hisia Anazokupa.

SIKILIZA

Tumia muda kuunganisha mambo ambayo umesoma, mambo ambayo umeomba na mambo ambayo umeimba na uone jinsi Bwana anavyovileta pamoja ili kuzungumza nawe.

SIFA

Msifu Bwana kwa muda ambao umekuwa naye na hisia ambazo amekupa. Msifuni kwa sifa zake tukufu.

Kutoka kwenye kitabu cha Dick Eastman cha The Hour that Changes the World (C) 2002 na Dick Eastman, Chosen Books, Grand Rapids, MI, kilichotumiwa kwa ruhusa.

JADILI

(10 min)

  1. Je, unaonaje kutumia lisali moja kwa maombi?
  2. Unahisi aje?
  3. Ulijifunza au kusikia chochote?
  4. Je! Maisha yangekuwaje kama ungefanya maombi ya aina hii kuwa kawaida?

READ

(5 min)

Orodha ya 100

Yesu alisema - "Nendeni mkafanye wanafunzi…" Na wafuasi wake walifanya vivyo hivyo.

Walienda kwa familia zao. Walienda kwa marafiki zao. Walienda kwa watu waliowajua mjini. Walienda kwa watu waliofanya kazi nao. Walienda.

Yesu alisema "Nendeni" nao wakatii. Na familia ya Mungu ikakua.

Mungu tayari ametupatia mahusiano tunayohitaji ili "twende na kufanya wanafunzi." Hao ni familia zetu, marafiki, majirani, wafanyakazi wenzetu na wanafunzi wenzetu - watu ambao tumewajua maisha yetu yote, watu ambao tumewajua hivi karibuni.

Kuwa waaminifu na watu ambao Mungu tayari ameweka maishani mwetu ni hatua nzuri ya kwanza katika kuzidisha wanafunzi. Na unaweza kuanza na hatua rahisi ya kuandika orodha.

Orodha ya watu 100 ni zana rahisi katika Seti Yetu ya Zana ya Zume inayozidisha wanafunzi.

SHUGHULI

(30 min)

Tengeneza orodha yako mwenyewe ya mia moja

Tengeneza orodha yako ya usimamizi wa mahusiano: andika watu walio katika miduara yako ya ushawishi. Weka alama kuonyesha ikiwa kila mtu ni mfuasi, bado si mwamini, au hajulikani.

Tumia muda kama kikundi ili kila mtu ajenge orodha yake mwenyewe. Unaweza kutumia karatasi au zana za kidijitali katika vifaa vyako vya mafunzo.

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
  • Ufafanuzi rahisi wa Mwanafunzi na Kanisa
  • Kupumua kwa Kiroho ni kusikia na kumtii Mungu
  • Mtumiaji wa Maisha dhidi ya Watumiaji
  • S.O.A.P.S. Kusoma Bibilia
  • Makundi ya Uwajibikaji
  • Jinsi ya kutumia Saa katika maombi
  • Usimamizi wa Jamaa - Orodha ya 100

KIKAO KALI CHA 2

INGIA

(1 min)

Waruhusu washiriki wote na mwezeshaji waingie.

Or six.zume.training/checkin and use code: 2341

OMBA

(5 min)

Omba na kumshukuru Mungu kwa njia ulizopitia Yeye katika kipindi kilichopita na mwalike Roho Wake Mtakatifu kuongoza wakati wako pamoja.

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Uchumi wa Kiroho
  • Maono Kutupa Baraka Kubwa Zaidi
  • Kufuatia Ufuasi - Kuongoza Mara Moja
  • Macho ya Kuona penye Ufalme Hauko
  • Injili na Jinsi ya Kushiriki
  • Ubatizo na Jinsi ya Kufanya
  • Ushuhuda wa Dakika Tatu
  • Meza ya Bwana na Jinsi ya Kuiongoza

READ

(5 min)

Uchumi wa Kiroho

Katika kikao hiki, tutaongea kuhusu UCHUMI wa KIROHO wa Mungu. Katika ulimwengu huu, watu wanajihisi wamezawadiwa wanapochukua, wanapopokea na wanapofaidika kuliko wenzao walio karibu nao.

Katika maandiko yake, Mungu anawaambia watu wake - Mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zangu sio njia zenu.

Mungu anatuonyesha kwamba katika uchumi wake wa Ufalme, tunazawadiwa sio kwa kile tunachopata - bali kwa kile kutoa.

Mungu anasema - nitawaokoa, nanyi mtakuwa baraka. Yesu anasema - Heri kutoa kuliko kupokea. Kutoa yale Mungu ametupa na kuwabariki wengine wakati Mungu anatubariki ni msingi wa KUPUMUA KIROHO tuliojifunza hapo awali.

Tunapumua NDANI na KUSIKIA kutoka kwa Mungu. Tunapumua NJE na KUTII yale tuliyoyasikia na KUSHIRIKI na wengine.

Tukiwa waaminifu KUTII na KUSHIRIKIANA yale BWANA ameshiriki nasi, basi hapo anaahidi kushiriki hata zaidi.

Yesu alisema - anayeweza kuaminiwa kwa vicache anaweza kuaminiwa kwa vingi. Hii ndiyo njia ya kufahamu kwa udani, ushirika wa karibu na kuishi maisha tele aliyotuumba Mungu tuyaishi. Hii ndio njia tunayoweza kutembea kutembea katika matendo mema ambayo Mungu ametupangia kufanya.

Ikiwa tunahitaji kuzawadiwa na zawadi kuu ya Mungu, Basi lazima tujizoeshe kwa mambo mawili aliyoahidi kubariki.

Ni lazima -

  • KUTII na KUSHIRIKIANA
  • FANYA na KUFUNDISHA
  • JIZOESHE na UPOKEZANE

-kila kitu Mungu anakueleza tukafanye.

Ikiwa tunataka wengine nao wapokee zawadi kuu ya Mungu, basi ni lazima tuwaonyeshe jinsi ya kufanya mambo hayo, pia. Hi ni sehemu muhimu ya kuwa mwanafunzi na sehemu muhimu ya kuwafanya wanfunzi.

  • Sisi ni WAFUASI na VIONGOZI
  • WANAFUNZI na WALIMU
  • TUMEBARIKIWA na sisi ni BARAKA

Mungu hataki tungojee hadi tumeelewa kila kitu kabla tuanze kutii na kushirikiana. Siku hiyo haitafika.

Mungu hatutarajii tukomae kabisa kabla tuanze kujizidisha. Anataka tujizidishe mara moja. Mungu anataka tutii yale tumejua tayari na kushirikiana yale tuliyoyasikia tayari.

Na kisha anataka tuwafundishe wengine kufanya hivyo. Baada ya yote - hiyo ni kutii na kushirikiana yale alituambia tukafanye. Hii ndio njia ya ukomavu na ukuaji.

JADILI

(10 min)

  1. Je, ni tofauti gani unazoona kati ya Uchumi wa Kiroho wa Mungu na njia yetu ya kidunia ya kufanya mambo kutendeka?
  2. Kwa nini unafikiri Yesu alichagua watu wa kawaida badala ya njia nyingine ya kushiriki habari zake njema?
  3. Je! Itachukua nini kwa wewe kujihisi vizuri kushiriki hadithi ya Mungu?

Yesu alisema, “Mtapokea nguvu akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu. Nanyi mtakuwa mashahidi wangu, mkihubiri habari zangu kila mahali, katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata miisho ya dunia."

JADILI

(10 min)

  1. Kitu gani hukujia mawazoni unaposikia amri ya Mungu ya kuwa "shahidi" wake na kusimulia hadithi yake?
  2. Kwa nini unafikiri Yesu alichagua watu wa kawaida badala ya njia nyingine ya kushiriki habari zake njema?
  3. Je! Itachukua nini kwa wewe kujihisi vizuri kushiriki hadithi ya Mungu?

Injili

Hakuna "njia bora zaidi" ya kusimulia hadithi ya Mungu (pia inaitwa Injili), kwa sababu njia bora itategemea nani unashiriki naye. Kila mwanafunzi anapaswa kujifunza kuelezea Hadithi ya Mungu kwa njia ambayo ni kweli kwa maandiko na inaeleweka kwa wasikilizaji wanaowashiriki.

Kagua mawasilisho mawili yafuatayo na uchague moja ya kufanya mazoezi.

READ

(5 min)

Wasilisho 1

Katika kikao hiki, tutajifunza jinsi ya kushirikiana HADITHI ya MUNGU - INJILI - kutoka Uumbaji hadi Hukumu, tangu mwanzo wa wanadamu hadi mwisho wa nyakati. Kuna njia nyingi za kushiriki hadithi ya Mungu.

Njia bora zaidi itategemea mtu unayeshiriki naye na maoni yake kuhusu ulimwengu na uzoefu wake wa kimaisha.

Mungu hutumia mioyo yenye nia ya kushiriki kutenda kwa mioyo yenye nia ya kusikia.

Ni kazi yake. Anatualika tu tukajiunge naye.

Njia moja ya kushiriki hadithi ya Mungu ni kwa kuelezea kilichotokea tangu Uumbaji hadi kwenye Hukumu mwa nyakati hizi.

Tunaposema hadithi ya Mungu kwa njia hii, tunaweza kuurefusha au kuufupisha, kwa kina au fupi fupi lakini iwe imeunganika na utamaduni wa mwenye anakusikiza.

Ili kusaidia kuelezea Hadithi Yake katika tamaduni tofauti na maoni ya ulimwengu, unaweza pia kuonyesha kwa mkono ambao hufanya iwe rahisi kujifunza na kufundisha.

Hapa kuna Hadithi ya Mungu ya Habari Njema -

Hapo mwanzo, Mungu aliumba ulimwengu na vitu vyote.

Aliumba MWANAUME wa KWANZA na MWANAMKE wa KWANZA. Akawaweka kwenye bustani nzuri. Aliwafanya kuwa SEHEHMU ya FAMILIA YAKE na UHUSIANO WA KARIBU pamoja nao.

Aliwaumba WAWEZE KUISHI pamoja. Hapakuwa kitu kama kifo.

Hata katika mahali hapa, mwanadamu alimuasi Mungu na kuleta DHAMBI na MATESO duniani.

Mungu akamfukuza mwanadamu kutoka kwenye bustani. Uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu ukakatizwa.

Sasa ikawa mwanadamu lazima afe.

Zaidi ya mamia ya miaka, Mungu alizidi kuwatuma WAJUMBE duniani. Waliwakumbusha wanadamu dhambi zao na pia kuwaeleza kuhusu UAMINIFU wa Mungu na AHADI zake za kumtuma MWOKOZI duniani.

Mwokozi angerejesha uhusiano wa karibu kati ya Mungu na wanadamu, mwokozi angemuokoa mwanadamu kutoka kwa kifo. Mwokozi atapeana uzima wa milele na kuokoa mwanadamu milele.

Mungu anatupenda sana hata wakati ulipotimia, alimtuma Mwanawe duniani ili awe yule Mwokozi.

Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Alizaliwa duniani kupitia bikira. Aliishi maisha makamilifu. Hakutenda dhambi.

Yesu aliwafundisha watu kuhusu Mungu. Alitenda miujiza mingi kudhihirisha uwezo wake. Alikemea pepo wengi. Aliponya watu wengi. Aliwafanya vipofu kuona. Aliwafanya viziwi kusikia. Aliwafanya viwete kutembea.

Yesu hata aliwafufua wafu. Viongozi wengi wa dini WALIHOFIA sana na kumchukia Yesu. Walitaka kumuua.

Kwa vile hakutenda dhambi, hakustahili kufa. Lakini ALIAMUA kufa kama DHABIHU kwetu sote. Kifo chake kilifunika dhambi za mwanadamu.

Baada ya haya, Yesu alizikwa kaburini.

Mungu aliona DHABIHU yake Yesu na kukubali. Mungu alionyesha kukubali kwake kwa kumfufua Yesu kutoka wafu siku ya tatu.

Mungu alisemba kwamba ikiwa TUTAAMINI na KUMPOKEA Yesu kama dhabihu ya dhambi zetu - TUKIACHANA na dhambi na KUMFUATA Yesu, Mungu HUTUTAKASA kwa dhambi zote na KUTUKARIBISHA tena katika jamaa yake.

Mungu humtuma ROHO MTAKATIFU aishi ndani mwetu na kutusaidia kumfuata Yesu.

TUNABATIZWA kwa maji kuonyesha na kuidhinisha uhusiano huu uliorejeshwa.

Kama ishara ya kifo tunazikwa ndani ya maji. Kama ishara ya maisha mpya tunainuliwa kutoka majini kumfuata Yesu. Wakati Yesu alipofufuka kutoka wafu, alikaa duniani siku arobaini.

Yesu aliwafundisha wafuasi wake kwenda kila mahali kufundisha kila mtu kuhusu habari njema ya wokovu wake.

Yesu alisema - NENDENI na MKAWAFANYE WANAFUZI mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwa BATIZA, kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na KUWAFUNDISHA kuyashika yote niliyowaamuru ninyi, tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata mwisho wa dahari.

Yesu AKAINULIWA juu mbele ya macho yao hata mbinguni. Siku moja, Yesu ATAKUJA TENA kwa njia hiyo hiyo.

Atawaadhibu milele wote ambao hawakumpenda na kumtii.

ATAWAPOKEA na KUWAZAWADI MILELE wote waliompenda na kumtii.

TUTAISHI MILELE pamoja naye katika Mbingu Mpya na Dunia Mpya.

NILIAMINI na NIKAPOKEA dhabihu iliyoandaliwa na Yesu kwa ajili ya dhambi zangu. Alinifanya kuwa msafi na kunirejesha kama sehemu ya jamaa ya Mungu. Ananipenda, nami nampenda milele katika ufalme wake.

Mungu anakupenda na anataka ukaipokee zawadi hii, pia. Je, ungependa kufanya hivyo sasa hivi?

READ

(5 min)

3-Miduara

Karibu tena kwenye Mafunzo ya Zume.

Katika kipindi hiki, tutajifunza jinsi ya kushiriki simulizi ya Mungu, yani injili, kwa kutumia zana inayoitwa Miduara Mitatu.

Kuna njia nyingi za kushiriki simulizi ya Mungu. Njia bora zaidi itategemea mtu unayeshiriki naye na mtazamo wake wa ulimwengu na yale aliopitia maishani.

Mungu hutumia mioyo iliyo tayari kushiriki kubadilisha mioyo iliyo tayari kusikia.

Ni kazi yake. Anatualika tu kujiunga naye.

Njia moja ya kushiriki simulizi ya Mungu ni kwa kushiriki mchoro rahisi tunaoita miduara mitatu.

Sote tunaishi katika ulimwengu uliovunjika. Tunaona na kusikia simulizi za kuteseka, kifo, vita, magonjwa na uraibu. Kila mahali. Lakini huo si mpango wa asili wa Mungu.

Mpango mkamilifu wa Mungu ni ulimwengu uliojaa upendo, furaha, umoja na amani.

Jinsi tulivyojiondoa kutoka kwenye mpango mkamilifu wa Mungu na kuingia katika hali ya kuvunjika ni kupitia kitu ambacho Biblia inakiita dhambi.

Dhambi ni kujitenga na njia ya Mungu na kufuata njia zetu wenyewe. Dhambi hututenganisha na Mungu. Dhambi hutuweka katika hali ya kuvunjika. Dhambi hutusababishia kifo cha kiroho.

Watu wanataka kujiondoa katika hali ya kuvunjika. Tunajaribu mambo mengi tofauti kujiondoa katika hali hiyo.

Baadhi yetu tulijaribu dawa za kulevya na pombe. Baadhi yetu hujaribu kujiondoa katika hali hiyo kupitia kazi nzuri au kujipatia pesa nyingi. Baadhi yetu hufikiri kwamba uhusiano fulani ndio suluhu. Wengine hata hujaribu dini. Tunafikiri tabia njema au kusaidia wengine kutatuweka huru.

Hayo yote hayawezi kurekebisha tatizo la kuvunjika.

Hata tunapohisi kana kwamba tumepata afueni kidogo, tunarudi pale pale tulipoanzia.

Ukweli mgumu ni huu, ikiwa bado tuko hapo, bado katika hali ya kuvunjika, maisha haya yanapoisha,Biblia inasema tutatenganishwa na Mungu milele.

Biblia inaita mahali hapo jehanamu.

Lakini Mungu hataki tusalie katika hali ya kuvunjika. Biblia inasema Mungu alitupenda sana kiasi kwamba alimtuma Mwanawe mwenyewe kutuletea suluhu.

Yesu alikuja duniani kufuta dhambi yetu na kutuondoa kwenye hali ya kuvunjika.

Lakini kwa jinsi gani? Yesu angewezaje kufanya hayo yote?

Yesu aliishi maisha makamilifu. Alikuwa mtu pekee ambaye hakuwahi kutenda dhambi. Yesu alikuwa mtu pekee aliyedumu katika mpango mkamilifu wa Mungu. Kisha akatoa maisha yake makamilifu na kuchukua nafasi yetu.

Alikufa msalabani ili kulipa gharama ya dhambi yetu.

Hivyo Yesu, Mwana wa Mungu, alifuta dhambi yetu kwa kifo chake.

Siku tatu baada ya Yesu kufa na kuzikwa, alifufuka kutoka kwa wafu.

Kwa sababu ya dhabihu yake kuu Mungu alimfanya Yesu kuwa Mfalme juu ya kila kitu mbinguni na duniani.

Mfalme Yesu alitoa suluhu ya kuvunjika kwa ajili yetu. Mungu alisema kwamba tukiacha dhambi zetu na kuamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu na tubatizwe kwa jina la Baba, Mwana na Roho Mtakatifu, Mungu antatufufua, kama Yesu, ili tuishi maisha mapya kama sehemu ya familia ya Mungu milele.

Kisha tunakuwa kielelezo cha maisha haya mapya katika ulimwengu uliovunjika tukimsubiri Yesu arudi, wakati atakapoumba mbingu mpya na dunia mpya, ambapo tunaweza kuwa pamoja naye milele tukiwa wakamilifu kabisa.

Mungu anataka tukue katika uhusiano wetu naye. Mungu anataka turejeshwe katika mpango wake mkamilifu wa asil.

Kama sehemu ya familia ya Mungu. Yesu alitupatia utume, sababu ya kuishi, na njia ya kuishi maisha bora iwezekanavyo.
Utume wa Yesu kwetu ni kuenda. Yesu anatutuma kama alivyofanya Baba yake. Mungu alimtuma katika hali ya kuvunjika ili awasaidie wengine kuwa huru ili nao pia wawe sehemu ya familia ya Mungu milele.

Katika ulimwengu huu wa miduara mitatu, kuna watu wa aina mbili tu. Watu ambao ni sehemu ya mpango mkamilifu wa Mungu, wakitekeleza utume wa Mungu wa ukombozi, wakisaidia kumuunganisha Mungu tena na familia yake ya milele au watu ambao bado wako katika hali ya kuvunjika wakijaribu kila kitu kujiweka huru, wakitumai kwamba kuna mtu atakayewakomboa.

Je, unajua uko wapi sasa? Je, unajua mahali unapotaka kuwa?

Kuna njia nyingi za kushiriki simulizi ya Mungu. Kilicho muhimu ni kushiriki.

Mungu hutumia mioyo iliyo tayari kushiriki, kubadilisha mioyo iliyo tayari kusikia.

Hiyo ni kazi yake. anatualika tu kujiunga naye.

SHUGHULI

(45 min)

kichwa: Shiriki Injili

Maudhui:

Hadithi ya Mungu: Mtindo wa Uumbaji hadi Hukumu

Hapo mwanzo, Mungu aliumba ulimwengu wote na vyote vilivyomo.

Alimuumba MWANAUME WA KWANZA na MWANAMKE WA KWANZA. Akawaweka katika bustani nzuri. Aliwafanya kuwa SEHEMU YA FAMILIA YAKE na kuwa na UHUSIANO WA KARIBU nao.

Aliwaumba WAISHI MILELE. Hakukuwa na kitu kama kifo. Hata mahali hapa pazuri, mwanadamu alimuasi Mungu na kuleta DHAMBI na MATESO duniani. Mungu AKAMFUKUZA mtu kutoka bustanini. Uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu ULIVUNJIKA. Sasa mwanadamu angekabiliana na MAUTI. Zaidi ya mamia ya miaka, Mungu aliendelea kutuma WAJUMBE duniani. Walimkumbusha mwanadamu dhambi yake lakini pia walimwambia juu ya UAMINIFU na AHADI ya Mungu ya kutuma MWOKOZI duniani.

Mwokozi Angeweza KURUDISHA uhusiano wa karibu kati ya Mungu na Mwanadamu. Mwokozi angemkomboa mwanadamu kutoka kwa kifo. Mwokozi angetoa UZIMA WA MILELE na kuwa na mwanadamu milele. Mungu anatupenda sana hata wakati ulipowadia, alimtuma Mwanawe ulimwenguni kuwa Mwokozi huyo.

Yesu alikuwa Mwana wa Mungu. Alizaliwa ulimwenguni kupitia bikira. Aliishi maisha makamilifu. Hakutenda dhambi kamwe. Yesu aliwafundisha watu kuhusu Mungu. Alifanya miujiza mingi akionyesha uwezo wake mkuu. Alitoa pepo wengi. Aliponya watu wengi. Aliwafanya vipofu waone. Aliwafanya viziwi wasikie. Aliwafanya viwete watembee. Yesu hata alifufua wafu. Viongozi wengi wa kidini WALITISHIWA na KUMWONEA WIVU Yesu.

Walitaka auawe. Kwa kuwa hakuwahi kutenda dhambi, Yesu hakupaswa kufa.

Lakini ALICHAGUA kufa kama SADAKA kwa ajili yetu sote. Kifo chake chenye uchungu kilifunika dhambi za wanadamu. Baada ya hayo, Yesu alizikwa kaburini. Mungu aliiona SADAKA ambayo Yesu aliitoa na kuikubali. Mungu alionyesha kukubalika kwake kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu siku ya tatu.

Mungu alisema kwamba ikiwa TUNAAMINI na KUPOKEA dhabihu ya Yesu kwa ajili ya dhambi zetu -- Tukigeukia mbali dhambi zetu na KUMFUATA Yesu, Mungu ANATUTAKASA kutoka kwa dhambi zote na ANATUKARIBISHA tena katika familia yake.

Mungu humtuma ROHO MTAKATIFU ​​kukaa ndani yetu na kutufanya tuweze kumfuata Yesu. TUMEBATIZWA katika maji ili kuonyesha na kuweka muhuri uhusiano huu uliorejeshwa.

Kama ishara ya kifo tunazikwa chini ya maji. Kama ishara ya maisha mapya tunainuliwa kutoka majini ili kumfuata Yesu.

Yesu alipofufuka kutoka kwa wafu, alitumia siku 40 duniani.

Yesu aliwafundisha wafuasi wake kwenda kila mahali na kutangaza habari njema ya wokovu wake kwa kila mtu ulimwenguni kote. Yesu alisema - Enendeni, MKAWAFANYE mataifa yote KUWA WANAFUNZI, MKIWABATIZA kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu; na KUWAFUNDISHA kuyashika yote niliyowaamuru. nitakuwa pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Ndipo Yesu ALIPULIWA Mbinguni mbele ya macho yao. Siku moja, Yesu ATARUDI TENA kwa njia ile ile aliyotoka. Atawaadhibu MILELE wale ambao hawakumpenda na kumtii. Atawapokea na kuwathawabisha MILELE wale waliompenda na kumtii. TUTAISHI MILELE pamoja Naye katika Mbingu Mpya na katika Dunia Mpya.

NILIAMINI na KUPOKEA dhabihu aliyoitoa Yesu kwa ajili ya dhambi zangu. Amenifanya kuwa safi na kunirudisha kama sehemu ya familia ya Mungu. Ananipenda, na ninampenda na nitaishi naye milele katika ufalme Wake. Mungu anakupenda na anataka upokee zawadi hii pia. Je, ungependa kufanya hivyo sasa hivi?

Fanya mazoezi ya uwasilishaji huu wa injili peke yako hadi uhisi vizuri kusimulia hadithi.

READ

(5 min)

Ubatizo

Yesu alisema: "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu…" Ubatizo - au Baptizo katika lugha ya Kigiriki -inamaanisha kuloweka au kuzamisha - kama wakati unapotia nguo rangi na inaloweka rangi hiyo na inatoka ikiwa imebadilika.

Ubatizo ni taswira ya maisha yetu mapya, yaliyoloweka taswira ya Yesu, na kubadilishwa ili kumtii Mungu. Ni taswira ya kifo chetu kwa dhambi, kama vile Yesu alivyokufa kwa ajili ya dhambi zetu; ni kuzikwa kwa maisha yetu ya zamani, kama vile Yesu alivyozikwa; ni kuzaliwa upya katika Kristo, kama vile Yesu alivyofufuliwa na anaishi leo.

Ikiwa hujawahi kumbatiza mtu hapo awali, huenda ikonekana kuwa jambo la kuogopesha, lakini halipaswi kuwa hivyo. Hizi hapa hatua rahisi. Tafuta maji yaliyosimama, yenye kina cha kutosha kuruhusu mwanafunzi mpya kuzamishwa ndani. Inaweza kuwa kidimbwi, mto, ziwa au bahari. Inaweza kuwa beseni kubwa au njia nyingine ya kukusanya maji.

Mruhusu mwanafunzi ashikilie mkono wako mmoja nawe umshikilie mgongoni na mkono wako mwingine.

Uliza maswali mawili kama haya ili kuhakikisha anaelewa uamuzi wake.

  • "Je, umempokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi?"
  • "Je, utamtii na kumtumikia kama Mfalme wako kwa maisha yako yote yaliyosalia?"

Ikiwa atajibu, "Ndiyo" kwa yote mawili, Basi sema kitu kama hiki:

  • "Kwa sababu umekiri imani yako katika Bwana Yesu, sasa nakubatiza kwa jina la Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu."

Msaidie kuingia kwenye maji, mzamishe kabisa kisha muinue tena juu.

Umembatiza mfuasi mpya wa Yesu - raia mpya wa mbinguni - mtoto mpya wa Mungu aliye hai. Sasa ni wakati wa kusherehekea!

Ubatizo - sakramenti ya kwanza ambayo Yesu aliwapa wafuasi wake na msingi wa Seti Yetu ya Zana ya Zume.

JADILI

(10 min)

  1. Je, umewahi kubatiza mtu?
  2. Je! Unaweza kufikiria kufanya hivyo?
  3. Ikiwa Agizo Kuu ni kwa kila mfuasi wa Yesu, je, hiyo inamaanisha kila mfuasi anaruhusiwa kubatiza wengine? Kwa nini au kwa nini?

Umuhimu wa anayekukumbusha-Umekua ukibatizwa?

Ikiwa sivyo, basi tunakuhimiza upange hili kabla hata ya kipindi kimoja zaidi cha mafunzo haya. Alika kikundi chako kuwa sehemu ya siku hii muhimu unaposherehekea kusema "ndiyo" kwa Yesu.

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Uchumi wa Kiroho
  • Maono Kutupa Baraka Kubwa Zaidi
  • Kufuatia Ufuasi - Kuongoza Mara Moja
  • Macho ya Kuona penye Ufalme Hauko
  • Injili na Jinsi ya Kushiriki
  • Ubatizo na Jinsi ya Kufanya
  • Ushuhuda wa Dakika Tatu
  • Meza ya Bwana na Jinsi ya Kuiongoza

UZURI WA ANAYEKUKUMBUSHA-Kundi lako litasherehekea Meza ya Bwana awamu inayokuja.Kuwa na hakika kusambaza(mikate na divai/mvinyo).

Take a Break

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Uchumi wa Kiroho
  • Maono Kutupa Baraka Kubwa Zaidi
  • Kufuatia Ufuasi - Kuongoza Mara Moja
  • Macho ya Kuona penye Ufalme Hauko
  • Injili na Jinsi ya Kushiriki
  • Ubatizo na Jinsi ya Kufanya
  • Ushuhuda wa Dakika Tatu
  • Meza ya Bwana na Jinsi ya Kuiongoza

READ

(5 min)

Ushuhuda wa Dakika Tatu

Yesu aliwaambia wafuasi wake -"Nyinyi ni mashahidi wa mambo haya." Kama wafuasi wa Yesu, sisi pia ni "mashahidi," -"tukishuhudia" kuhusu kile ambacho Yesu amefanya maishani mwetu. Simulizi yako kuhusu uhusiano wako na Mungu inaitwa ushuhuda wako. Kila mtu ana simulizi yake. Hii ni fursa ya kuifanyia mazoezi simulizi yako.

Chagua mfuasi mmoja au wawili wa kufanya nao mazoezi kisha chagua majina matano kwenye orodha yako ya watu 100. Hakikisha unachagua watu kutoka kwenye kikundi cha "wasio Wakristo" au "hali ya kiroho haijulikani." Fanya mazoezi ya ushuhuda wako -simulizi yako kumhusu Yesu - kwa kufanya washirika wako wa mazoezi waigize kama mmoja wa wale watu watano uliowachagua kwenye orodha yako. Fanya mazoezi ya kuandaa simulizi yako ili iwe mahususi kwa kila mmoja wa watano hao. Unapaswa kuweza kushiriki simulizi yako iliyofupishwa ndani ya takriban dakika tatu.

Kuna njia nyingi za kuandaa simulizi yako, Lakini zifuatazao ni baadhi ya njia ambazo tumeona zikiwa bora kwa wengine: Unaweza kutoa kauli rahisi kuhusu kwa nini ulichagua kumfuata Yesu. Hii ni bora kwa muumini mpya. Unaweza kushiriki kuhusu maisha yako ya "awali" na ya "sasa" -jinsi maisha yako yalivyokuwa kabla ya kumjua Kristo na jinsi maisha yako yalivyo sasa. Ni njia rahisi na yenye nguvu.

Unaweza kushiriki kuhusu wakati "umekuwa naye" na "kabla ya kuwa naye" jinsi maisha yako yalivyo "ukiwa na Yesu" ma jinsi yangelivyokuwa "bila Yesu." Aina hii ya simulizi yako ni bora ikiwa ulimjua Yesu ukiwa kijana mdogo.

Ukishamaliza kushiriki, acha mshirika wako wa mazoezi pia ashiriki. Endeleeni mkipokezana mpaka nyote wawili mmalize watu hao watano. Ungependa kuwa na athari kubwa zaidi?

Unaposhiriki simulizi yako, inasaidia kuichukulia kama sehemu ya mchakato wenye sehemu tatu:

  • Simulizi yake - Mwombe mtu unayeongea naye ashiriki kuhusu safari yake ya kiroho.
  • Simulizi yako - Kisha shiriki ushuhuda wako ukizingatia yale mtu huyo alipitia.
  • Simulizi ya Mungu - Hatimaye shiriki simulizi ya Mungu kwa njia inayofungamana na mtazamo, maadili na vipaumbele vya mtu huyo.

Na ikiwa una wasiwasi kuhusu jinsi ya kuanza - tumia njia rahisi.

Shiriki tu kauli kuhusu kwa nini uliamua kumfuata Yesu. Mungu anaweza kutumia simulizi yako kubadilisha maisha, lakini kumbuka - wewe ndiye utakayeisema.

Ushuhuda wako wa Dakika Tatu ni zana nyingine rahisi katika Seti Yetu ya Zana ya Zume.

SHUGHULI

(30 min)

kichwa: Ushuhuda wa Dakika Tatu

Maudhui:

Aina Tatu za Msingi za Ushuhuda

Kuna njia nyingi za kuunda hadithi yako, lakini hizi ni baadhi ya njia ambazo tumeona zikifanya kazi vizuri:

  • Taarifa Rahisi - Unaweza kushiriki taarifa rahisi kuhusu kwa nini ulichagua kumfuata Yesu. Hii inafanya kazi vizuri kwa muumini mpya kabisa.
  • Kabla na Baada - Unaweza kushiriki hadithi yako "kabla" na "baada ya" - maisha yako yalikuwaje kabla ya kumjua Yesu na maisha yako yalivyo sasa. Rahisi na yenye nguvu.
  • Pamoja na Bila - Unaweza kushiriki hadithi yako ya "na" na "bila" - maisha yako yalivyo "pamoja na Yesu" na jinsi ingekuwa "bila Yeye". Toleo hili la hadithi yako hufanya kazi vizuri ikiwa ulikuja kuamini katika umri mdogo.

Sehemu Tatu za Kushiriki Ushuhuda Wako

Unaposhiriki hadithi yako, ni muhimu kuifikiria kama sehemu ya mchakato wa sehemu tatu:

  • Hadithi Yao - Uliza mtu unayezungumza naye kushiriki kuhusu safari yao ya kiroho.
  • Hadithi Yako - Kisha shiriki Ushuhuda wako kulingana na uzoefu wao.
  • Hadithi ya Mungu - Hatimaye shiriki hadithi ya Mungu kwa njia inayounganishwa na mtazamo wao wa ulimwengu, maadili na vipaumbele.

Si lazima Ushuhuda wako uwe mrefu au ushiriki maelezo mengi ili uweze kuleta matokeo. Kwa kweli, kuhifadhi hadithi yako kwa takriban dakika 3 kutaacha wakati wa maswali na mazungumzo ya kina. Ikiwa una wasiwasi kuhusu jinsi ya kuanza - iwe rahisi. Mungu anaweza kutumia hadithi yako kubadilisha maisha, lakini kumbuka - wewe ndiye unayeweza kuisimulia.

READ

(5 min)

Baraka Kuu, Kubwa, na Kubwa Zaidi

Katika awamu hii, tutazungumzia kuhusu ukuu wa Mungu, ukuu zaidi na Baraka kuu na vile utakavyowapa wengine Baraka hizo. Wakati mtu anapochagua kumfuata Yesu, unamsaidiaje kwa kupata mwongozo kwa njia iliyo sawa?

Unawasaidiaje kuwa wazalishaji katika ufalme wa Mungu na siwatumiaji?

Unawasiadiaje kupokea baraka yote ambayo Mungu anapendelea kuwapa?

Ninaanza kwa kuwambia hivi…

  • Ni Baraka kumfuata Yesu.
  • Ni Baraka kuu kuwaongoza wengine kumfuata Yesu.
  • Ni Baraka kuu kuanza familia mpya ya kiroho.
  • Ni Baraka iliyo kuu zaidi kuandaa wengine kuanza familia mpya za kiroho.

Umechagua kumfuata Yesu na Mungu amekubariki.

Nahitaji upokee Baraka za Mungu, Baraka kuu, Baraka kuu mno, zaidi pia. Naweza kukuonyesha.

Ikiwa wanahitaji kufahamu zaidi, nitahitaji wao kutengeneza orodha ya watu 100 ambao tayari wanawafahamu.

Baadaye nitawauliza kuchagua watu watano kutoka kwa orodha hiyo watu watano ambao hawamjui Yesu, watano wangependa kushiriki neno mara moja.

Ni Baraka kufuata Yesu. Ungemshirikisha nani tena katika Baraka hizi?

Nawafundisha jinsi ya kutoa ushuhuda - na hadithi ya vile Mungu anafanyakazi katika maisha yao - Nawapa maelekezo ya kueneza injili-hadith kuhusu kile Mungu amefanya duniani. Nawafundisha kuhusu Baraka za Mungu zilivyo kuu, kuu zaidi, na ajabu.

Nitahitaji kuwapa mazoezi ya kufanya kwa kila kundi la watu watano walio wachagua kushiriki nao. Kwanza kuhusu hadithi yao wenyewe. Halafu hadithi kuhusu Mungu. Hatimaye baraka za Mungu.

Kila wakati najifanya kuwa mmoja wa hao watano walio katika orodha yao.

Kila wakati wanaelezea hadithi yao. Wanaelezea hadithi kuhusu Mungu. Wananialika kuwa mfuasi wa Yesu pia. Wanafundisha kuhusu ukuu wa Mungu, ukuu zaidi, na Baraka za Mungu pia.

Kila wakati nawahoji ili kupata mapendekezo ambayo nafikiria mtu anaweza kupendekeza. Baada ya mazoezi, nawaomba tukutane tena-ikiwezekana siku mbili baadaye- ili kutaathimini mwendo wao unavyoendelea.

Nahitaji kuwapa muda wa kutosha ili kukutana na watu watano walio waorodhesha, ila sitaki kuwapa muda mrefu wasije wakasahau na kufutilia mbali hatua hiyo.

Siku zote nawaomba anuani yao au namba ya simu ili kuendelea kuwasiliana nao.

Naomba pamoja nao ili Mungu awape maneno sahihi vile wanavyoendelea kushiriki nami.

Siku mbili baadaye, tunakutana na kuwa na mazungumzo nao kuhusu vile wanavyoendelea kushiriki.

Ikiwa hawajashirikisha wengine, najitolea kufanya mazoezi nao. Najitolea kutembea nao ikiwa wale watano inawezekana wawemo. Nafanya kulingana na uwezo wangu ili kuwafanya waanze kushiriki.

Ila sitazungumzia vitu vipya. Nitawapa muda unaofaa wa kuwa waaminifu kwa yale wamejifunza.

Ikiwa watakataa au kuwa visingizi, ninaomba Mungu ikiwa ni kweli "udongo warutuba" ambao utazalisha katika ufalme wake au ikiwa kuna mwingine sehemu nyingine ambapo naweza kuwekeza.

Ikiwa walishirikisha wengine -tunasherekea.

Hata kama hakuna katika orodha hiyo ambaye hakuamini, ninafurahia maana WAMESIKIA KUTII na KUSHIRIKISHA WENGINE. Hapo ni kuwa mwaminifu.

Na vile wamekua waaminifu kwa vichache, ninafurahia kuwapa zaidi.

Nawafundisha kuhusu UBATIZO na kuwapa silaha nyingine wanaweza kutumia kama njia ya mambo na kubuni kikundi kuwauliza kuchagua watu wengine kutoka orodha ya watu mia moja- watu ambao hawamjui au hawamfuati Yesu.

Baadaye nafanya mazoezi nao kama awali - na hadithi yao na ya Mungu na Baraka za Mungu. Halafu tunaomba.

Sasa ikiwa watajadiliana na mmoja wao aamini katika orodha hiyo basi kwa kweli TUTASHEREHEKEA!

Familia ya Mungu inaendelea kukuwa kubwa.

Mara kwa mara nawauliza ikiwa wamezungumzia Baraka kuu, kuu na kuu mno sababu hii ndio hufanya familia ya Mungu kukua.

Ikiwa hawakuzumgumzia kuhusu Baraka za Mungu, basi tunaanza tena--Baraka, jinsi gani mfuasi mpya wa Yesu anaweza kutengeneza orodha, wanawezaje kuzungumzia hadithi zao, zungumzia Mungu na Baraka za Mungu--vivyo hivyo mwanafunzi wa Yesu anaweza kujifunza na kuzungumzia pia.

Hatimaye baada ya kufanya mazoezi, nawatuma tena kwa waumini wapya ili waweze kuendelea kushiriki nao.

Na inakuaje kwa yule ambaye ameshiriki na mmoja katika orodha hiyo ameamini na walizungumzia kuhusu mibaraka?

Ikiwa yanafanyika ninajawa na FURAHA SANA.

Watu kama hawa neno la Mungu linawaita "udongo wa rutuba"--yeyote anayekua katika njia ya familia ya Mungu ni wakuu kuliko vile sijawahi waona.

Popote ninapopata mtu kama huyu, nafanya mpango wakukutana nao. Ninawekeza zaidi katika kukua kwao kwa kiroho.

Nawafundisha somo jipya kama UBATIZO na jinsi ya kuanza THELUTHI TATU ya makundi. Sasa wanaweza anza kukua familia ya kiroho- kwanza kwa wale waumini wapya wa Yesu.

Vile walivyo waaminifu, nimejawa na furaha kuzungumza zaidi kulingana na uwezo wangu na kuona kile ambacho Mungu atafanya baadaye. Siku zote hatua moja kwa wakati mmoja. Siku zote nawapa muda wakujifunza, kutii na kuwapa wengine kile wanachojua.

Pia ninaomba na mtu huyu-kulingana na uwezo wangu-Na kushukuru Mungu kuniruhusu kushiriki na kujifunza nao na daima kuomba Mungu kuwapa wote baraka zake kuu.

JADILI

(10 min)

  1. Je, huu ndio kielelezo ulichofundishwa ulipoanza kumfuata Yesu kwa mara ya kwanza? Ikiwa sivyo, ni nini kilikuwa tofauti?
  2. Baada ya kuwa mwenye Imani, ilikuchukua muda gani kabla uanze kuwafanya wengine kuwa wanafunzi?
  3. Unafikiria nini kitatendeka ikiwa wafuasi wapya wataanza kushiriki na kufundisha wengine, mara moja?

READ

(5 min)

Uwanafunzi wa Watoto wa Bata

Karibu tena kwa mafundisho ya Zume

Katika awamu hii, tutajifunza jinsi vifaranga wa bata wanavyojifunza kuelea kwa maji. Ni mbinu yakutufanya kuelewa kanuni mbili za kuanzisha uanafunzi.

Je umewahi kuona kundi la vifaranga wa bata wakitembea ?

Haijalishi popote ulipo duniani vifaranga wote wa bata siku zote wanafanana.

Mama wa vifaranga hao huwaongoza huku wanawe wakimfuata moja kwa moja kwa mpangilio. Mama hutangulia huku vifaranga hufuata nyuma taratibu.

Ila ukiangalia kwa makini na karibu , utaona kuna jambo linalotendeka. Kila kifaranga anashughulikia maswala mawili kwa wakati mmoja.

Kila kifaranga wa bata ni mfuasi, kwa sababu anafuata mwenendo wa mamake anatembea mbele yao. Na kwa wakati mmoja na uliokubalika.

Kila bata ni kiongozi, kwa sababu anaongoza huku vifaranga wakiwa nyuma yake.

Je bata ni mfuasi au kiongozi? Bata ni kiongozi na mfuasi.

Ni sababu tosha za bata akiwa anatembea ana majukumu yote ya kutengeneza wanafunzi.

Mungu anahitaji familia kukua kwa kiwango cha juu -na anatarajia kila mtu kuwa kiongozi, kila muumini kuwa mshiriki, na kila mwanafunzi kuandaa wanafunzi wengine kwa wakati mmoja.

Katika mtego mmoja tunaoangukia, kama mwanafunzi na anayetengeneza wanafunzi, ni imani potovu ambayo tunahitaji kujua kila kitu, au kila kitu, kabla hatujashiriki katika jambo lolote.

Ila hivyo sivyo uanafuzi hufanyika.

Wanafunzi ni kama vifaranga wa bata. Kuwa kiongozi, hawahitaji kujua kila kitu. Ilimradi wawe hatua moja mbele.

Mungu anahitaji familia yake kuwa waaminifu na anatarajia kila kiongozi kuwa mfuasi, kila anayeshiriki kuwa muumini, kila anayetengeneza wafuasi kuwa mwanafunzi kwa wakati mmoja.

Mtego mwingine tunaoangukia, kama mwanafunzi anayetengeneza wafuasi, nimafundishaye uongo ambayo mtu au mahali kila mmoja anajua ikiwa tutafuata baadaye itagundulika ni mtego.

Ila hiyo ni mbinu ya uanafunzi.

Katika ufalme wa Mungu tuna mama wa bata mmoja ambaye tunamfuata wote ni Yesu.

Hakuna mmishenari, wala mhubiri au profesa wa seminari ila Yesu tu ndiye anastahili kiwango cha imani yetu.

Yaliyosalia kwetu ni mchakato.

Kuna mmoja siku zote aliye karibu na Yesu ambaye twaweza kumfuata. Na kuna mmoja aliye mbali twaweza kumuongoza. Haijalishi nyadhifa zetu au roho zetu siku zote roho zetu zishikamane na Kristo.

Katika Bibilia Paulo aliyeandika mambo mengi katika agano jipya na aliyeanzisha makanisa mengi hakuandika "nifuate" anasema nifuate vile ninavyomfuata Kristo.

Paulo alijua kukuza kila mahali mnako wanafunzi walistahili kujua vile vile, kila kiongozi katika ufalme wa Mungu lazima awe mfuasi na wote tuamfuata Yesu.

Pia katika Bibilia Paulo anaandika:

"Kile umekisikia kutoka kwangu …waambie wengine kwa uaminifu, wale watakaowafundisha wengine pia.

Paulo alijua kuwa na wafuasi kila mahali na alijua kila kitu ambacho wanafunzi wanatakiwa kujua. Kila mfuasi katika ufalme wa Mungu sharti awe kiongozi na aongoze kama Yesu kutoa uhai kwa ajili ya wengine.

Ukihitaji kuona familia ya Mungu ikiongezeka kwa kasi na kwa uaminifu, fikiria kuhusu uanafunzi unaotengezwa kama bata kuwa mfuasi na kiongozi kwa wakati mmoja.

JADILI

(10 min)

  1. Ni sehemu gani moja ya uanafunzi (kusoma / kuelewa Biblia, kuomba, kushiriki Hadithi ya Mungu, nk) ambayo unataka kujifunza zaidi kulihusu? Ni nani anayeweza kukusaidia kujifunza?
  2. Nini sehemu moja ya uanafunzi ambao unafikiri unaweza kushirikiana na wengine? Ungeliishiriki na nani?

READ

(5 min)

Macho ya Kuona penye Ufalme Hauko

Katika wamu hii tutajifunza jinsi ambapo ongezeko la uanafuzi hufanyika mbali na kwa haraka wakati wanapoona ufalme wa Mungu hauko mbali.

Kama binadamu tunafikiria kuhusu kazi na vitu ambavyo tunavyona,Tunaviita vya ukweli. Vile vitu vilivyo .Ila ufalme unakua kwa kasi ikiwa tutazingatia kuona vitu visivyoonekana. Vitu ambavyo havipo. vitu ambavyo havipo

Kuna sehemu nyingi karibu nasi ambapo mapenzi ya Mungu hayajafanyika duniani kama vile mbinguni kuna mwanya mkubwa ambapo kuna kuvunjika kwa mioyo ,kusalitiana,machungu,dhiki na hata kifo vimekuwa mambo ya kawaida katika maisha ya kila siku.

Kila mwanafunzi-mfuasi wa Yesu anahitaji kuwa na uwezo wa kuona si tu sehemu ufalme wa Mungu ulipo ila mahali ufalme wa Mungu hauonekani.

Kazi ya ufalme wa Mungu ni kupenyeza sehemu ambazo kuna mianya ,sehemu za giza ili kuleta nuru katika sehemu hizo hasa tunamoishi katika ulimwengu huu.

Tunaweza kuona awamu mbili za ufalme wa Mungu ---kupitia watu tunaowajua na wale ambao huajakutana nao.

Kwanza kwa watu tunaowajua -katika mwendo wa mausiano ya marafiki na familia ,tunaofanya kazi nao,tunaosoma pamoja, majiriani na wengine wengi.

Hivi ndivyo hadithi ya Mungu inavyoenda kwa kasi sana. Tunawapenda na kuwajali sababu tayari tunawafahamu tayari. Ni kawaida.

Yesu alisimulia kisa cha tajiri aliyejipenda-mroho katika maisha na sasa alipata adhabu kuzimu. Tajiri anamsihi kwa kumtuma Lazaro Nenda kwa babangu awape onyo ndugu zangu watano ili wasije mahali hapa nilipo pa dhiki.

Yesu anatuonyesha jinsi walafi wanaoteseka wanao upendo kwa walio karibu nao.

Watu tunaowajua wamewekwa karibu nasi na Mungu ili tuonyeshe upendo wa Mungu na anahitaji tuwapende. Tunahitaji kuwa mawakili wema kwa uhusiano wa upendo na uvumilivu.

Wanafunzi wanaongezeka wakati wanajihisisha na watu wa Mungu waliokaribu nao na wana mipango ya kufanya jambo kuwahusu.

Unaweza kusaidia kwa kuwajali ili kutoa mchango wa kuwajenga na kutoa mpango wa kuongeza uzalishaji katika hatua chache.

Inafanyika hivi-Wafahamishe waandikwe watu 100 wanaowajua. Waambie sasa wagawe watu hao katika makundi matatu.

  • Wale wanaomfuata Yesu
  • Wale ambao hawamfuati Yesu.
  • Wale ambao hawana uhakika ikiwa wanafuata Yesu au la.

Kwa wafuasi-wanafunzi wanaweza kuwatia moyo kwa kuongezeka na kuwa waaminifu.

Kwa wasioamini-wanafunzi wanaweza kujifunza jinsi ya kushirikiana nao na kuwasilisha katika upendo wa Mungu

Na kwa wale wasio na hakika-wanafunzi watajifunza jinsi ya kuwekeza kwa muda na kujifunza zaidi.

Kuna njia nyingine ambapo tunaona ufalme wa Mungu haujafikiwa kwa watu ambapo hatujakutana nao.

Kuna watu wako nje ya mahusiano yetu-watu tusiowajua,majirani ambapo hatusemi nao zaidi ya neno 'habari' kwa wafanyabiashara wakiume au wakike tunakutana nao wanaopita katika barabara zetu, wageni vijijini, mji na jiji kamwe hatuwatembelei.

Yesu alisema-wafanye wanafunzi kote ulimwenguni.

Yesu alisema-utawaeleza kuhusu mimi kwanza Yerusalemu,Judea,Samariana ulimwenguni kote.

Kushiriki na watu unaowajua ni njia ambayo hadithi ya Mungu usambaa kwa haraka.

Kushiriki na watu usio wajua ni njia mojawapo neno la Mungu uenda mbali.

Ikiwa tunawapenda watu tusio wajua na kuwajali basi si kawaida ila ni nguvu za kiungu na ushahidi wa kazi ya Roho mtakatifu katika maisha yetu.

Wanaopendwa na Mungu ni wachache, wa mwisho na waliopotea. Hao ndio huwamwagia roho yake tena na tena.

Ikiwa tunahitaji kuwa kama Mungu,basi awa ndio tuahitaji kuwekeza katika maisha yetu.

Mungu ametuamrisha twende. Na sehemu ya kwenda ni kuenda na si wale walio karibu nasi bali wale walio katika giza nene la kiroho kwenye pembe zote za dunia hii-watu ambao hawawahi lisikia jina Yesu.

Neno la Mungu linasema-Mungu hapendi kiburi huwarehemu wanyenyekevu.

Kama wafuasi wa Yesu sharti tuwape wema vile anavyotupa-kuwa mnyenyekevu kwa wasio na uwezo na waliopotea.

Wanafunzi wanaongezeka wakati wanapojihusisha watu ambapo amewaka katika maisha yao.

Wanafunzi wanaongezeka hata zaidi wakati wanapojihusisha kwa watu wa Mungu ambapo hawapo karibu nao. Hata hivyo wanahitaji mpango wao.

Unaweza kusaidia kuongeza wanafunzi kwa kujali wengine ,kujenga mpango mdogo wa kutoa mafundisho kwa watu ambapo Mungu tayari ameandaa mioyo yao.

Yesu alisema-unapokaribia makazi sema "Mungu bariki nyumba hii na amani" Ikiwa watu wanaoishi humo ni wapenda amani basi maombi yako ya amani yatawabariki. Ila si wa amani, maombi yako yatakurudia.

Mwito kwa yeyote aliyeitwa tayari na Mungu aliyeandaliwa kusikiliza mtu wa amani-Aliyewajibishwa na ujumbe wa Mungu na mwaminifu kwa kutii na kushirikisha wengine.

Katika sehemu zingine tunajua machache badala ya kuwajali wengine kama marafiki,jamii, wafanyakazi wenzetu, tunaosoma pamoja nao, tunafundisha mtu jinsi atakavyo wafikia wenzake.

Matokeo mazuri siku zote huja wakati tunalenga waliowaaminifu. Kumbuka uaminifu utokana na kutii kile ambacho Mungu anatuambia na kuwapa wengine.

Watu waaminifu wanaotii na kuwapa wengine ni kama mchanga wa rutuba ambao Yesu anazungumzia kuhusu.

Yesu alisema-mbengu chache zilianguka kwenye udongo wa rutuba sehemu ambapo mimea huzaana mara thelathini au sitini ama mara mia moja vile zilivyo tawanyika.

  • Watu wa Mungu hawana roho ngumu ya kukataa neno la Mungu.
  • Waaminifu hawakati tama hata kama wanateswa au wakati kuwa mgumu.
  • Watu waaminifu hawatatiziki kwa matatizo ya ulimwengu huu au utajiri usio dumu.
  • Watu waaminifu ni kama wamepagawa sawa na yule mtu wa Gerasene aliyetii na kuwajulisha wengine kile Yesu alimuonyesha.

Mtu mwaminifu ni yule anayetii na kuwapa wengine papo hapo uzalisha wengi, wengi wanaotaka kumjua Yesu.

Tufungueni macho yetu tuone mahali ufalme haupo na kuzuru nje kupitia watu tunao wajua na watu tusio wajua na hivyo ndivyo wanafunzi wanaongezeka na ufalme wa Mungu unakuwa na kuenda kasi.

JADILI

(10 min)

  1. Unajihisi vizuri kuishiriki na nani - - - watu ambao tayari unawafahamu au wale ambao hujawahi kukutana nao, bado?
  2. Unafikiri hiyo ni nini?
  3. Unaweza kuboreshaje kushiriki kwako na watu ambao hujihisi vyema nao?

READ

(5 min)

Meza ya Bwana na Jinsi ya Kuiongoza

Yesu alisema -_ "Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu." _

Ushirika Mtakatifu au "Meza ya Bwana" ni njia ya kusherehekea uhusiano wetu wa karibu na unaoendelea na Yesu.

Hii ni njia rahisi ya kusherehekea -

Mnapokusanyika pamoja kama wafuasi wa Yesu, tumieni muda katika kutafakari kwa utulivu, mkizingatia na kuungama dhambi zenu kwa ukimya.

Mwombe mtu asome kifungu hiki kutoka kwenye Maandiko -- " Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate; naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, "Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu." (1 Wakorintho 11:23-24)

Peana mkate ulioandaa kwa ajili ya kundi lako na mle.

Endelea na somo -- " Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, 'Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.'" (1 Wakorintho 11:25)

Peana juisi au divai ulioandaa kwa ajili ya kundi lako na mnywe.

Maliza somo -- " Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo." (1 Wakorintho 11:26)

Mmeshiriki pamoja Meza ya Bwana.

Sherekeheni kwa sala na nyimbo - nyinyi ni wake naye ni wenu!

Meza ya Bwana sakramenti takatifu kutoka kwa Kanisa la Kwanza na sehemu muhimu ya Seti Yetu ya Zana ya Zume.

SHUGHULI

(10 min)

kichwa: Meza ya Bwana

Maudhui:

Unapokusanyika kama wafuasi wa Yesu:

  1. Tumia muda katika kutafakari kwa utulivu, ukizingatia kimya kimya na kuungama dhambi zako.
  2. Unapokuwa tayari, mwambie mtu asome kifungu hiki kutoka katika maandiko -- Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa ninyi, ya kwamba Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate; na akiisha kushukuru, akaumega, akasema, Huu ni mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. (1 Wakorintho 11:23-24)
  3. Toeni mkate mliowatengea kundi lenu, mle.
  4. Endelea kusoma -- Vivyo hivyo akakitwaa kikombe, baada ya kula, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi, kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu.' (1 Wakorintho 11:25)
  5. Shiriki juisi au divai ambayo umetenga kwa ajili ya kikundi chako, na unywe.
  6. Maliza kusoma: Kwa maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hicho, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. (1 Wakorintho 11:26)

Sherehekea kwa maombi au kuimba. Umeshiriki Meza ya Bwana. Wewe ni Wake, na Yeye ni wako!

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Uchumi wa Kiroho
  • Maono Kutupa Baraka Kubwa Zaidi
  • Kufuatia Ufuasi - Kuongoza Mara Moja
  • Macho ya Kuona penye Ufalme Hauko
  • Injili na Jinsi ya Kushiriki
  • Ubatizo na Jinsi ya Kufanya
  • Ushuhuda wa Dakika Tatu
  • Meza ya Bwana na Jinsi ya Kuiongoza

KIKAO KALI CHA 3

INGIA

(1 min)

Waruhusu washiriki wote na mwezeshaji waingie.

Or six.zume.training/checkin and use code: 3455

OMBA

(5 min)

Omba na kumshukuru Mungu kwa njia anazofanya kazi kupitia ushuhuda wa watu wake. Alika Roho wake Mtakatifu kuongoza wakati wako pamoja.

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Mtu wa Amani na Jinsi ya Kupata Moja
  • Uaminifu ni bora kuliko Ujuzi
  • Mfano wa Maombi ya BURE
  • Kutembea kwa Maombi na Jinsi ya Kufanya
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

READ

(5 min)

Kutembea kwa Maombi

Neno la Mungu lasema tunapaswa kufanya "dua, na sala, na maombezi, na shukrani, kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu; ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli."

Kutembea kwa maombi ni njia rahisi ya kutii amri ya Mungu ya kuombea wengine. Kutembea Ukiomba kunamaanisha jinsi inavyosikika - kuomba kwa Mungu huku ukitembea.

Badala ya kufumba macho yetu na kuinamisha vichwa vyetu, tunafumbua macho yetu ili tuone mahitaji yanayotuzunguka na kuinamisha mioyo yetu na kuomba msaada wa Mungu kwa unyenyekevu. Mnaweza kutembea kwa maombi katika vikundi vya watu wawili au watatu au unaweza kufanya hivyo peke yako.

Mkiwa kikundi - jaribuni kuruhusu kila mmoja aombe kwa sauti, mwe na mazungumzo na Mungu kuhusu kile kila mmoja anaona na mahitaji ambayo Mungu ataleta mioyoni mwenu.

Ukiwa peke yako - omba kimoyomoyo au kwa sauti ikiwa unaomba na mtu uliyekutana naye njiani.

Zifuatazo ni njia nne za kujua kile unachoweza kuombea Unapotemeba ukiomba:

  • Kutazama -- Je, unaona nini? Ukiona kitu cha mtoto cha kuchezea kwenye bustani, huenda ukapata msukumo wa kuombea watoto wa mtaa huo, familia au shule za eneo hilo.
  • Utafiti -- Je, unajua nini? Ikiwa umesoma kuhusu mtaa huo, huenda unajua kitu kuhusu watu wanaoishi hapo, au ikiwa eneo hilo lina tatizo la uhalifu au ukosefu wa haki. Ombea mambo hayo na umwombe Mungu aingilie kati.
  • Ufunuo -- Roho Mtakatifu huenda akagusa moyo wako au akakuletea wazo akilini kwa ajili ya hitaji mahususi la maombi. Sikiliza - na uombe!
  • Maandiko -- Huenda ulisoma sehemu ya Neno la Mungu ukijitayarisha kutembea au unapotembea, Roho Mtakatifu anaweza kukuletea andiko fulani akilini. Omba kuhusu kifungu hicho na jinsi kinavyoweza kuathiri watu wa eneo hilo.

Zifuatazo ni NYANJA TANO ZA USHAWISHI ambazo unaweza kuzingatia unapotembea kwa maombi:

  • Serikali - Tafuta na uombee vituo vya Serikali kama vile mahakama, majengo ya tume au ofisi za utekelezaji wa sheria. Ombea ulinzi wa eneo hilo, haki na hekima ya kiungu kwa ajili ya viongozi wa eneo hilo.
  • Bishara - Tafuta na uombee vituo vya kibiashara kama vile maeneo yanayoshughulikia fedha au ya kununua bidhaa. Ombea uwekezaji wenye uadilifu na usimamizi bora wa rasilimali. Ombea haki ya kiuchumi na fursa za kiuchumi na watoaji wakarimu na wacha Mungu wanaoweka watu mbele ya faida.
  • Elimu - Tafuta na uombee vituo vya Elimu kama vile shule na majengo ya usimamizi, vyuo vya mafunzo anwai, vyuo vya kijamii na vyuo vikuu. Ombea waelimishaji waadilifu wa kufunza ukweli wa Mungu na wanaolinda akili za wanafunzi wao. Omba kwamba Mungu aingilie kati kupinga juhudi zote za kueneza uwongo au mkanganyo. Omba kwamba sehemu hizo zitatuma raia wenye hekima walio na moyo wa kutumika na kuongoza.
  • Mawasiliano - Tafuta na uombee vituo vya Mawasiliano kama vile vituo vya redio na televisheni na wachipashaji wa magazeti. Omba kwamba simulizi ya Mungu na ushuhuda wa wafuasi wake uenezwe kote mjini na kote duniani. Omba kwamba ujumbe wake uwasilishwe kupitia vyombo vyake kwa watu wengi na kwamba watu wa Mungu kila mahali wataona kazi ya Mungu.
  • Mambo ya Kiroho - Tafuta na uombee vituo vya kiroho kama vile majengo ya kanisa, misikiti au hekalu. Omba kwamba kila mtafutaji wa kiroho atapata amani na faraja katika Yesu na hatapotoshwa au kukanganywa na dini yoyote ya uwongo.

Hatimaye, zifuatazao ni njia tano za kuombea watu unaokutana nao Unapotembea ukiomba:

Unapotembea na kuomba, kuwa macho ili kuona fursa na usikilize misukumo ya Roho wa Mungu kuhusu kuwaombea watu na vikundi unavyokutana navyo njiani. Unaweza kusema, "Tunaombea jamii hii, kuna kitu chochote mahususi tunachoweza kuombea?" Au sema, "Naombea eneo hili. Unajua kitu chochote mahususi tunachoweza kuombea?" Baada ya kusikiliza jibu lao unaweza kuuliza kuhusu mahitaji yao binafsi. Wakiyataja, yaombee mara moja. Bwana akikuongoza, unaweza kuombea mahitaji mengine pia.

Tumia neno la Kiingereza BLESS kukusaidia kukumbuka njia 5 tofauti za kuomba:

  • Mwili (afya)
  • Kazi (kazi na fedha)
  • Kihisia (motisha)
  • Kijamii (mahusiano)
  • Kiroho

Mara nyingi, watu watashukuru kwamba unajali vya kutosha kuwaombea.

Ikiwa mtu husika si Mkristo, maombi yako huenda yakafungua mlango wa mazungumzo ya kiroho na fursa ya kushiriki simulizi yako na simulizi ya Mungu. Unaweza kumwalika kuwa sehemu ya kikao cha kujifunza Biblia au kuruhusu kifanyike nyumbani kwake.

Ikiwa mtu husika ni Mkristo unaweza kumwalika kujiunga nawe kutembea mkiomba au umfunze jinsi ya kutembea akiomba ukitumia hatua rahisi kama kuombea nyanja za ushawishi au maombi ya BLESS ili kukuza familia ya Mungu hata zaidi.

Kutembea Ukiomba zana nyingine rahisi katika Seti Yetu ya Zana ya Zume.

READ

(5 min)

Mtu wa amani

Karibuni tena kwa mafundisho ya Zume.

Katika kikao cha awali tulijulishwa kwa wazo la mtu wa Amani. Katika kikao hiki tutaingia kwa undani zaidi kuona huyu mtu anaweza kuwa nani na jinsi ya kufahamu ikiwa umepata mmoja. Mtu wa amani kwa haraka anaweza kusaidia kuzalisha wanafunzi - hata mahali ambapo wanafunzi wa Yesu ni wachache na wako mbali mbali.

Wakati Yesu alipotuma wafuasi wake katika maeneo mapya ili kuwafanya wanafunzi, aliwapa amri rahisi lakini yenye maarifa.

Yesu alisema - - Wasichukue pesa za bindoni, wala mkoba, wala viatu; wasisalimie mtu njiani. Nyumba yoyote waingiapo, kwanza semeni, 'Amani na iwe ndani ya nyumba hii.' Kukiwemo na mtu wa amani mle ndani, amani yenu itakaa juu yake; kama sivyo, itawarudieni. Kaeni humo, mkila na kunywa watachowapa; kwa kuwa mfanyakazi anastahili ujira wake. Msiende nyumba hadi nyumba.

Lakini hiyo yote inamaanisha nini?

Wakati tunapofikiria kuwafanya wanafunzi, mawazo yetu kwanza yatakuwa - tuwe na pesa za kutosha, tuchague lengo dhahiri, na tuwe na mpango dhahiri wa utekelezaji. Ikiwa Yesu alisema - "NENDA," sharti "tuende" na tuzidi kuenda! Ambia kila mtu! Kila mahali! Kila wakati!!!

Lakini Yesu, katika amri yake, hakuonekana kuwa na wasiwasi juu ya fedha na juhudi, na kujihusisha sana na alilolenga.

Yesu alitaka wafuasi wake kuangalia - na kuwekeza - kwa mtu wa amani.

Ikiwa unataka kufanya wanafunzi mahali ambao sio wengi - au pengine hata - wapo, hapo kumpata mtu wa Amani ni kitu cha maana unaweza kufanya.

Mtu wa Amani ni:

  • Mtu ambaye yuko WAZI kusikia Hadithi yako,Hadithi ya Mungu na Habari Njema ya Yesu.
  • Mtu ambaye ni MKARIMU na ANAKUKARIBISHA nyumbani kwake au mahali pa kazi au kujiunga na jamaa na marafiki katika jambo.
  • Mtu ambaye ANAJUA WENGINE (au ANAJULIKANA NA WENGI) na mwenye furaha kuunganisha kundi ndogo au umati.
  • Mtu ambaye ni MWAMINIFU na HUSHIKIRIKIANA yale aliyojifunza na wengine - hata baada ya wewe kuwaacha.

Katika Biblia, tunajifunza kwamba Yesu na wafuasi wake walikutana na Watu wa Amani - ghafla.

Katika nchi ya Wagerasi, Yesu alikutana na mtu mwenye pepo na aliishi peke yake akiwa amefungwa minyororo. Hatuwezi kumdhania kuwa Mtu wa Amani, lakini alikubali kumsikiza Yesu. Alikuwa MKARIMU na hata KUMKARIBISHA Yesu kule alikuwa anaishi. Alikuwa anajulikana vizuri na angeweza kuvutia umati kwa urahisi - hata kama tabia yake ni mbaya.

Na Yesu aliona kwamba yeye ni MWAMINIFU na hapo AKASHIRIKI naye pamoja na jamaa yake jamii yake na nchi yake yote kile Yesu anamaanisha kwake. Kwa kweli, wakati Yesu aliporudi pale katika eneo lile, umati mkubwa ulijikusanya, wakiwa na furaha ya kuona Mtu ambaye wamesikia mambo mengi kumhusu.

Kule Samaria, Yesu alikutana na mwanamke kisimani. Akawa wazi kwa Yesu, kwa nia ya kuwa MKARIMU na kujibu ombi lake la kunywa maji. Tunajifunza kwamba alikuwa na waume watano na bado alikuwa anaishi na mume mwingine, na kwa hivyo katika mji huu mdogo, alikuwa na hakika kwamba ANAJULIKANA KWA WATU WENGINE. Na Yesu akaongea naye, alikuwa MWAMINIFU na AKASHIRIKIANA - kwa haraka ambapo hata mji mzima ukamuomba Yesu abaki pale akashiriki nao, pia. Alikubali.

Kwa hivyo, ikiwa Mtu wa Amani anaweza kuishi mahali popote, na kufanya chochote, na kuwa mtu ambaye tunamjua au tunakutana naye - tunawezaje kupata mmoja?

Hapa kuna njia tatu rahisi - -

Tunaomba mapendekezo kutoka kwa watu katika jamii - Ni nani anayeaminika hapa? Je, kuna mtu hapa ambaye anafikiria watu wengine kwanza kabla ya kujifikiria? Ikiwa tutasikia jina hilo tena na tena - tutajaribu kukutana naye, kushirikiana wazo la kiroho, na kuona ikiwa wako tayari kusikia na kushiriki.

TUNAJITOA kuombea mtu wakati tunafanya Maombi ya Kutembea, au kazini, au michezoni - wakati wowote panapo fursa - na kisha kubadilisha maombi hayo kuwa mazungumzo ya kiroho.

TUNAINGIZA mawazo ya kiroho katika mazungumzo ili kuona ikiwa Mungu anateda katika maisha ya mtu. Ikiwa wako tayari na wenye nia, basi tunauliza ikiwa wanaweza kukusanya kikundi kujadiliana hata mengi.

Uliza mapendekezo, KUJITOLEA kuomba, INGIZA mawazo ya kiroho. Hizi zote ni njia ambapo tunaweza kuanzisha mchakato wa kupata Mtu wa Amani. Na haijalishi tunawapataje, kumbuka Yesu alisema tunastahili kutumia wakati mwingi wa kufanya wanafunzi na Mtu wa Amani.

Ni rahisi kufikiria kwamba ni "haki" kutumia wakati mchache kwa kila mtu, kwa usawa. Lakini Yesu alisema - na kuonyesha - hataki tuwe watu wa ki juju kwa kila mtu bali kupeana kwa undani kwa wachache.

Yesu mara nyingi alivutia umati, lakini Biblia inatuambia tena na tena kwamba Yesu angelijitenga kutoka kwa umati na kutumia wakati wake na wafuasi wake wa karibu kumi na wawili.

Mara kadhaa, Yesu angetumia wakati mwingi na kundi dogo la watu watatu peke.

Ikiwa Yesu, ambaye alikuwa na uwezo zaidi, nguvu nyingi, mamlaka zaidi, nidhamu, hekima, maarifa, kuelewa na huruma alichagua kutumia wakati akiwekeza kwa wachache na kuambia wafuasi wake nao wafanye vivyo hivyo, je, si ni ya muhimu tunapaswa kufuata na kushirikiana kwa mfano wake mkamilifu?

Mtu wa Amani

Sio rahisi kuzipata - huenda ni moja kwa elefu. Lakini kama hazina iliyofichwa inayostahili kutafutwa, thamani yao ya kukuza jamaa ya Mungu haipimiki.

JADILI

(10 min)

  1. Je! Mtu mwenye "sifa mbaya" (kama mwanamke Msamaria au mtu aliyekuwa na pepo huko Garasi) anaweza kuwa Mtu wa Amani? Kwa nini au kwa nini sivyo?
  2. Je! ni jumuiya au sehemu gani ya jamii iliyo karibu nawe inayoonekana kuwa na uwepo mdogo (au hakuna) wa Ufalme?
  3. Je, Mtu wa Amani (mtu ALIYE WAZI, MKARIMU, ANAWAJUA WENGINE na ANASHIRIKI) angewezaje kuharakisha kuenea kwa Injili katika jumuiya hiyo?

SHUGHULI

(10 min)

Kichwa: Maombi ya BARAKA

Maudhui:

Mfumo wa maombi ya BARAKA

Mfumo wa maombi ya BARAKA unatoa njia tano unazoweza kuwaombea watu unaokutana nao wakati wowote, lakini hasa unapotembea katika maombi.

  • Mwili - afya
  • Kazi - kazi na fedha
  • Kihisia - ari
  • Mahusiano ya kijamii
  • Kiroho - kumjua na kumpenda Mungu zaidi

SHUGHULI

(90 min)

Kichwa: Kutembea kwa Maombi

Maudhui:

Vyanzo vinne vinavyoweza kuongoza maombi yako:

  1. ANGALIZO Unaona nini? Ukiona kichezeo cha mtoto kwenye uwanja, unaweza kuchochewa kuombea watoto wa ujirani, familia au shule katika eneo hilo.
  2. UTAFITI Je! Unajua nini? Ikiwa umesoma kuhusu ujirani, unaweza kujua jambo fulani kuhusu watu wanaoishi huko, au ikiwa eneo hilo linakabiliwa na uhalifu au ukosefu wa haki. Omba juu ya mambo haya na umwombe Mungu atende.
  3. UFUNUO Roho Mtakatifu anaweza kuugusa moyo wako au kuleta wazo akilini kwa ajili ya hitaji fulani au eneo fulani la maombi. Sikiliza - na uombe!
  4. MAANDIKO Huenda umesoma sehemu ya Neno la Mungu katika kujitayarisha kwa ajili ya kutembea kwako au unapotembea, Roho Mtakatifu anaweza kukukumbusha Maandiko. Omba kuhusu kifungu hicho na jinsi kinavyoweza kuwaathiri watu katika eneo hilo.

Maeneo matano ya ushawishi ya kuzingatia maombi:

  1. SERIKALI Tafuta na kuombea vituo vya serikali kama vile mahakama, majengo ya tume au ofisi za utekelezaji wa sheria. Ombea ulinzi wa eneo hilo, haki na hekima ya kimungu kwa viongozi wake.
  2. BIASHARA NA BIASHARA Tafuta na uombee vituo vya biashara kama vile wilaya za kifedha au eneo la ununuzi. Ombea uwekezaji wa haki na uwakili mzuri wa rasilimali. Ombea haki ya kiuchumi na fursa na watoaji wakarimu na wacha Mungu wanaotanguliza watu mbele ya faida.
  3. ELIMU Tafuta na uombee vituo vya elimu kama vile shule na majengo ya utawala, vituo vya mafunzo ya ufundi stadi, vyuo vya jamii na vyuo vikuu. Sali ili waelimishaji waadilifu wafundishe kweli ya Mungu na kulinda akili za wanafunzi wao. Omba kwamba Mungu aingilie kati katika kila juhudi kuendeleza uwongo au machafuko. Omba kwamba maeneo haya yatume raia wenye busara ambao wana moyo wa kutumikia na kuongoza.
  4. MAWASILIANO Tafuta na uombee vituo vya mawasiliano kama vile vituo vya redio, vituo vya televisheni na wachapishaji wa magazeti. Ombea Hadithi ya Mungu na ushuhuda wa wafuasi Wake kuenea katika jiji zima na duniani kote. Omba kwamba ujumbe Wake utolewe kwa njia Yake kwa umati Wake na kwamba watu wa Mungu kila mahali waone kazi ya Mungu.
  5. UROHO Tafuta na uombee vituo vya kiroho kama vile majengo ya makanisa, misikiti au mahekalu. Omba kwamba kila mtafutaji wa kiroho apate amani na faraja katika Yesu na asikengeushwe au kuchanganyikiwa na dini yoyote ya uwongo.

OMBA

(5 min)

Kabla hujatoka kwenye shughuli yako ya Kutembea kwa Maombi, hakikisha unaomba pamoja na kikundi chako ili kumaliza muda wako pamoja.

Asante Mungu kwa kuwa anawapenda waliopotea, wa mwisho na wa mwisho - tukiwemo sisi!

Mwambie auandae moyo wako na moyo wa wale utakaokutana nao wakati wa matembezi yako kuwa wazi kwa kazi Yake.

Take a Break

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Mtu wa Amani na Jinsi ya Kupata Moja
  • Uaminifu ni bora kuliko Ujuzi
  • Mfano wa Maombi ya BURE
  • Kutembea kwa Maombi na Jinsi ya Kufanya
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

READ

(5 min)

Uaminifu

Katika kikao hiki, tutajifunza jinsi UAMINIFU ni kipimo bora cha ukuaji wa kiroho kuliko maarifa na mafundisho. Kuna mawazo mawili ambayo yamesababisha matatizo kadhaa kanisani, leo.

Kwanza ni kwamba wazo la ukuaji wa kiroho wa mtu umeunganishwa na jinsi unavyolielewa neno la Mungu. Wao hufanya kana kwamba ni IMANI YA HAKI - au imani halisi - ni kipimo kizuri cha imani ya mtu.

La pili ni kwamba wazo la uwezo wa mtu wa kuongoza unahitaji "mafundisho kamili" kabla waanze kuhudumia. Wao hufanya kana kwamba MAARIFA KAMILI - nicho kipimo cha uwezo wa mtu wa kuhudumu.

Shida na wazo la kwanza - ni kuegemea - IMANI KAMILI - au "imani ya haki" ni kwamba Shetani, mwenyewe, anaelewa maandiko kuliko mwanadamu yeyote. NENO la MUNGU linasema - unaamini kwamba kuna Mungu mmoja. Sawa! Hata mapepo wanaamini hivyo - na kutetemeka.

Kipimo kizuri cha ukuaji wa kiroho wa mtu ni IMANI ZOEFU - "zoezi la haki".

Tunapaswa kujihusisha sana na UAMINIFU katika KUTII na KUSHIRIKIANA kuliko kupima ukuaji wa kiroho kwa yale tunayoyajua pekee.

Shida na wazo la pili - ya kwamba mtu lazima awe amesoma zaidi kabla wawe viongozi kwamba hakuna aliyefundishwa zaidi.

Yesu alituma viongozi wachanga ambao bado wana mengi ya kujifunza ili waweze kufanya kazi zingine muhimu katika Ufalme.

Neno la Mungu linasema - Yesu aliwaita wafuasi wake wote kumi na wawili na akawapa uwezo juu ya mapepo wote na magonjwa. Kisha akawatuma kutangaza kuhusu Ufalme wa Mungu na kuwaponya wagonjwa.

Watu hawa walitumwa kabla Petro kushiriki imani yake kwamba Yesu ni Mwokozi - kitu kile tunachukulia kama hatua ya kwanza ya imani. Na hata baada ya kutumwa Yesu bado alimkemea Petro mara kadhaa kwa makosa na Petro baadaye bado alimkana Yesu. Wafuasi wengine walibishania uongozi kati yao na kazi ya kila mmoja katika Ufalme wa Mungu ujao.Wote walikuwa na mengi ya kujifunza, lakini Yesu aliwaweka wote kufanyanya kazi, kushirikia mtu walichojua tayari.

Uaminifu - ni zaidi mafundisho - ni kitu ambacho kinchoweza kuanzishwa unapoanaza kumfuata Yesu.

Uaminifu - Zaidi ya mafundisho.

Ikiwa TUNATII na KUSHIRIKIANA na wengine yale tumesikia, sisi ni waaminifu.

Ikiwa tutasikia na TUKATAE kutii na kushirikiana, sisi si waamini.

Tunapozidisha wanafunzi, hebu na tuhakikishe kwamba tunapima vitu vilivyo sahihi.

JADILI

(10 min)

  1. Fikiria juu ya amri za Mungu ambazo tayari unazijua. Je, wewe ni "mwaminifu" kiasi kipi wa kuitii na kushiriki mambo hayo?

READ

(75 min)

3/3 Mkutano wa Kikundi

Karibu tena kwa mafundisho ya Zume. Katika kipindi hiki tutajifunza jinsi theluthi 3/3 (FAHAMU: TAMUKA HIVI "Theluthi-Tatu") Kikundi ni njia ya kukutana kinachowasaidia wafuasi wa |Yesu kuweza kusaidiana wenyewe esnspomfuata Yesu kwa karibu.

Yesu alisema - - "kwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo paop hapo katikati yao." Hiyo ni ahadi yenye nguvu, na ambacho kila mfuasi wa Yesu anastahili kuiona kama faida. Lakini mnapokutana kama kundi, Je, mnatumiaje wakati wenu?

Theluthi 3/3 Kundi kile ambacho hugawanyisha wakati wao pamoja katika sehemu tatu ili waweze kujizoeza kutii baadhi ya mambo muhimu yanayoamurishwa na Yesu.

Inatumika hivi:

  • Theluthi tatu ya kwanza ya kundi kinatumika kwa kuangalia yale yaliotendeka tangia tuwe pamoja.
  • Theluthi ya kati ya kundi kinatumika kwa Kuangalia Hekima ya Mungu na mwelekeo wake katika maandiko, majadilianao na maombi.
  • Theluthi ya mwisho ya wakati wa kundi hutumika kwa Kuangalia mbele jinsi tunavyoweza kutumia na kutii yale tumejifunza.

Katika kikao hiki kundi lako litaongozwa kupitia toleo fupi la theluthi tatu la kundi kuwasaidia kujitayarisha kwa masimulizi kamili katika maisha halisi.

Kumbuka kikao kwa kupumua kiroho? Vuta hewa ndani, sikia kutoka kwa Mungu. Achilia hewa itoke, tii yale unayoyasikia na ushirikishe wengine. Hicho ndicho theluthi 3/3 hasa.

Kundi la theluthi 3/3 ni kile ambacho kinagawanyisha wakati wake katika sehemu tatu, ili waweze kujizoeza kusikia kutoka kwa Mungu na kutii na kushirikiana baadhi ya mambo muhimu yanayoamurishwa na Yesu.

Kikao hiki chafaa kudumu lisaa limoja, na litaenea kwa haraka. Ukiwa na kikundi kikubwa ama kikundi kipendacho majadiliano ya kindani, unaweza ukauliza mmoja wa kikundi asaidie kuweka wakati kwa kutumia saa.

Kwa Maisha halisi, hatua hizi zitaenea pole pole, lakini unapo fanyia mazoezi hakikisha unazidi kuendelea ndiposa usiishiwe na saa. Usiruke hatua zozote - zote ni muhimu!

Kumbuka kwamba kundi la theluthi 3/3 si sawa na Masomo ya Biblia - hiyo ni kwa kusudi! Tumia uzoefu huu kama fursa ya kujifunza njia mpya ya kukutana na yale yote mazuri Mungu amepangia wakati wenu mkiwa pamoja.

Mko tayari? Na tuanza!

KUTAZAMA NYUMA

Muda yetu ya kwanza ya theluthi ya kwanza tutaitumia kwa kuangalia nyuma kwa kujaliana na kutoa shukrani, kwa kushikiana mapambano yetu na kuombea wanachama wengine wa kundi letu. Tutaangalia kuona ikiwa kila mtu katika kundi amepata fursaya kutii na kushiriki pamoja na wengine yale waliyojifunza wakati wa mwisho tuliokuwa pamoja.

Hatua ya Kwanza - "Kutoa Shukrani."

Mpa kila mtu muda wa kushiriki na wengine chochote anatoa shukrani kwalo. Bonyeza kidude cha video cha kusimamisha na ufanye hivyo sasa hivi...Je, bado uko pale? Kweli, tunataka ubonyeze kidude cha kusimamisha, ili kila mmoja katika kundi lako aweze kushiriki na wengine kile anachomshukuru Mungu kwalo. Tutakuwa papa hapa mkirejea.

Hatua ya Pili - "Kushiriki Jitihadi zako" and "na Kuombeana."

Hebu sasa kila mtu katika kundi lako ashiriki na wengine kile wachopambana nalo. Mtu mwingine anaweza kuombea yale wanayoyashiriki na wengine. Bonyeza kidude cha kusimamisha, kisha shiriki na uombe.

Hatua ya Tatu - "Kuzingatia Kundi."

Kila wakati mkutanapo, mnastahili kuchukua wakati wenu kufikiria ni kwa nini muko pamoja - kumpenda Mungu, kuwapenda wengine, kumshiriki Yesu, na kuwasaidia wengine kumshiriki pia pia.

Kunazo njia nyingi ambazo kundi linaweza kuzinatia katika huduma, lakini katika kikao hiki cha mazoezi acha mtu asome kwa sauti Mathayo 22:37-38. Bonyeza kidude cha kusimamisha, kisha asome.

Hatua ya Nne - "Kuthibitisha."

Hii ni sehemu ambayo baadhi ya makundi wanataka kuruka kwa sababu inamaanisha kuuliza maswali ambayo wakati mwingine inaweza kuwa ngumu.

Tafadhali usiiruke.

Yesu aliwapenda wafuasi wake hata kuwauliza maswali magumu. Ikiwa tunataka kuwa kama Yesu, tuwapende wengine hata kuweza kufanya vile. Katika hatua hii, mtu mmoja katika kundi anapeana ripoti kuhusu ikiwa alitii yale alisikia Mungu akimweleza kufanya wakati wa mwisho mlipokuwa pamoja.

Katika kila kipindi cha Zume, tumeweka ahadi hizi katika hatua yetu ya kuangalia mbele ambapo tunakuomba uitii, mkaishiriki na muombe. Tumeweka kielelezo cha uajibikaji ya hatua ya kuangalia nyuma ambapo tunakuomba Ukaangalie ahadi hizo.

Ikiwa hamkuwa mnatumia muda mwingi kwenye hatua hizi hadi sasa katika mafundisho, huu ni wakati mzuri wa kuanza.

Sehemu ya kumpenda Mungu na kutii anachotuambia. Sehemu ya kupendana ina maana kumsaidia mtu kutii wanachosikia kutoka kwa Mungu.

Upendo inamaanisha kuchukulia ahadi za mtu kwa uzito - na kuwaonyesha upendo kwa neema - wote kwa wakati moja.

Bonyeza kidude cha kusimamisha na ambia kila mtu ajibu maswali yafuatayo?

  • Je, umetii aje yale umejifunza hadi sasa?
  • Umefundisha nani yale umejifunza?
  • Umeshiriki na nani hadithi yako ama hadithi ya Mungu tangu tuwe pamoja kama kikundi?

Tunapomalizia sehemu ya kutazama nyuma ya kundi letu la theluthi 3/3, hapa kuna kitu cha kusaidia vikao vyenu kuboreka zaidi:

KIDOKEZO CHA MAFUNDISHO YA ZUME

Wakati mwingine katika kundi, mtu mmoja anaweza kuwa ndiye mnenaji kila wakati. Hili lisitendeke. Kila mtu katika kundi ako na thamani, kwa hivyo hakikisha kwamba kila mmoja anapata nafasi ya kushirki.

Ikiwa wengine hawapati nafasi ya kuongea, basi kwa upole elezea yule anayenena zaidi kwamba kila mtu anapaswa kusikizwa.

KUTAZAMA JUU

Katikati ya wakati ya theluthi tatu yetu pamoja, tunamkaribisha Roho Mtakatifu wa Mungu kutuongoza kuelewa vyema Neno la Mungu.

Kwa sauti ya juu tutasoma fungu kutoka kwenye Biblia kisha tuulize na kujibu maswali rahisi kama kundi kutusaidia kuchunguza na kuelewa vizuri malengo na mipango ya Mungu.

Hatua ya Kwanza - Mkaribishe Roho Mtakatifu wa Mungu Aongoze

Chukua muda mfupi ili uombe. Ongea na Mungu kwa urahisi na kwa ufupi. Omba Roho wake Mtakatifu akufundishe kutoka kwenye kifungu ambacho unaenda kukisoma. Bonyeza kidude cha kusimamisha kisha omba.

Hatua ya Pili - Soma Neno la Mungu na Ukaulize Maswali

Mtu mmoja katika kundi asome kutoka kwenye Biblia. Kwenye kikao hiki cha mazoezi, soma Luka 18:9-14. Akishamaliza kusoma, kundi linapaswa kujibu maswali mawili:

  • Ulipenda nini kuhusu kifungu hiki?
  • Changamoto ilikuwa nini ama kilichokuwa kigumu kuelewa?

Ikiwa kunao wanafuzi - watu ambao hawasomi vizuri ama wanaopenda kujifunza kwa kusikia - katika kundi lenu, hakikisha umesoma kifungu angalau mara mbili.

Bonyeza kidude cha kusimamisha, soma na ujibu maswali.

Sasa acha mtu mwingine akasome kifungu hicho mara ya pili, kisha kundi lijibu maswali haya mawili:

  • Je, unaweza kujifunza kuhusu watu katika kifungu hiki?
  • Je, tunaweza kujifunza nini kumhusu Mungu kutoka kifungu hiki?

Kumbuka kuzingatia kifungu kwa njia rahisi!

Hiyo ndio mwisho ya sehemu ya Kutazama Juu ya theluthi 3/3 yetu, na hapa kuna kitu cha kusaidia vikao vyenu kuwa hata bora zaidi:

KIDOKEZO CHA MAFUNDISHO CHA ZUME

Wakati unapojifunza Kumbuka kukaa katika vifungu vya Neno la Mungu, zingatia maneno yake badala ya vitabu vingine, walimu, au maoni. Badala ya kuuliza, "Unafikiri hii inamaanisha nini?" uliza "Kifungu hiki kinasema nini?"

Ikiwa kuna mtu katika kundi lenu ambaye angependa kufundisha, kwa upole mkumbushe kwamba Roho Mtakatifu wa Mungu na neno kamili linaweza kufundisha kundi. Sote tuko hapa kwa minajili ya kufifunza, pamoja. Na usiogope ukimya ama kusimamishwa kiasi kwa majadiliano. Mungu anafanya kazi hata kukiwa kimya.

Endelea kilenga Neno Lake, baki kwa kifungu, mtumainie Mungu kutenda mengine.

KUANGALIA MBELE

Katika theluthi tatu ya mwisho ya wakati wetu, tunazingatia kuangalia mbele jinsi tunavyoweza kutii na kuwafundisha wengine yale tumejifunza kutoka kwa neno la Mungu.

Kila mwanachama wa kikundi anauliza Mungu maswali machache rahisi kisha anaongojea majibu yake kwa maombi. Kisha tunashiriki na kutekeleza ahadi zetu na kuomba kumaliza wakati, wetu pamoja.

Hatua ya 1 - Kuombea kusudi lake Mungu

Kila mmoja katika kundi lenu aombe kimya na amwulize Mungu maswali haya:

Mungu, naweza kutii na kumiaje yale unanifundisha?

  • Naweza kufundisha akina nani kutokana na kifungu hii ili waweze kujifunza na kukupenda zaidi?
  • Je, ungependa nishiriki na nani ushuhuda wangu au Habari njema za Yesu?

Bonyeza kidude cha kusimaisha kisha ukaombe.

Omba Roho Mtakatifu wa Mungu akupe majibu maalum, majina maalum na hatua maalum ambazo unaweza kuchukua wakati huu na wakati kundi lenu litakapo kutana tena.

Hatua ya 2 - Kukusanya ahadi

Uliza kila mtu katika kundi lako kushiriki na wengine yale waliyoyasikia kutoka kwa Bwana kwa kila swali. Huenda mtu hakusikia lolote kutoka kwa Bwana kwa swali moja, mbili, au hata zote tatu. Wanaweza tu kutoa ripoti kwamba hawakusikia lolote.

Lakini kumbukeni, kundi lazima lisikie kutoka kwa Bwana. Yesu alisema - "Kondoo wangu husikia sauti yangu." Na hatua zako za utiifu zilivyo, itakuwa rahisi kuzitii kabla tukutane tena.

Bonyeza kidude cha kusimamisha, kisha shiriki na wengine yale uliyoyasikia.

Shatua ya 3 - Kujizoeza na mpango wako

Kabla muda wenu pamoja kuisha, gawanyeni kundi lenu la theluthi 3/3 kwa vikundi viwili ama vitatu vidogo vidogo na mjaribu kufanya yale mmesikia Bwana anawaeleza mkafanye.

Kumbukeni - kujizoeza sio kutii, kujifundisha ama kushiriki, bali inawatayarisha kuwa tayari kufanya mambo hayo vizuri sana.

Kila kundi ndogo likamilishe zoezi lake kwa maombi. Ombea hao watu hasa na mipango Mungu ameweka ndani ya mioyo yenu.

Ikiwa muko na wanafunzi wasioweza kuandika katika kundi lenu, tenga wakati wa kuwasomea tena vifungu vya neno la Mungu mliosoma awali.Hili litasaidia kundi lote kuwa tayari kushiriki na wengine watakaokutana nao katika mikutano.

Bonyeza kidude cha kusimamisha, kisha mjigawanye katika vikundi kujizoeza na kuomba. Mtu yeyote asiyekuwa na shughuli maalum na ajizoeze kushiriki hadithi ya ushuhuda wake au hadithi ya Mungu.

Unapoleta kundi lako pamoja tena, chukua muda wako kusherehekea! Sasa mmekamilisha sehemu ya Kuangalia Mbele na mmejizoeza theluthi 3/3 ya muundo wa kikundi.

Kundi litaendelea kujizoeza bila mwongozo huu wa video katika vikoa vya baadaye. Hakikisha mnabadilishana ili wengine nao waongoze mchakato. Sio lazima uwe mwalimu mwenye ujuzi, fuata tu hatua hizi rahisi.

Kabla hamjaondoka, hapa kuna kidokezo kimoja cha kusaidia vikao vyenu kuwa hata bora zaidi:

KIDOKEZO CHA MAFUNDISHO CHA ZUME

Kote duniani, makundi ya theluthi 3/3 huwa wanashiriki meza ya Bwana pamoja, au chakula na mazungumzo ya kawaida kama sehemu ya wakati wao pamoja.

Mungu alitupa ushirika kama huu - - kujifunza kwa maksudi na kukua na kuishi kwa maksudi na uhusiano kusaidia kutupa nguvu, kutuhimiza, na kutujenga ili tuwe kama Mwanawe, Yesu.

Na ni hivyo - kundi lako sasa limejizoeza sehemu zote tatu - Tunaangalia nyuma kuhakikisha yale tumetimiza tangia wakati wa mwisho tulipokutana, Kuangalia Juu ili kuelewa yale Mungu anavyo kwetu kujifunza pamoja katika wakati huu, na tunaangalia Mbele kuweka vitedo vyote ambavyo Mungu ameweka ndani ya mioyo yetu wakati tulikuwa mbali mbali.

Kikundi cha theluthi 3/3 - njia rahisi ya kukutana inayotusaidia kuwa kama Yesu.

JADILI

(10 min)

  1. Je, umeona tofauti yoyote kati ya Kundi la 3/3 na Masomo ya Biblia au Kundi ndogo ambayo umekuwa sehemu yake (au umewahi kusikia) katika siku za nyuma? Ikiwa ndivyo, utofauti hizo zinaathiri kundi hizo kiaje?
  2. Je, Kundi la 3/3 linaweza kuchukuliwa kuwa Kanisa Rahisi? Kwa nini au kwa nini?

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Mtu wa Amani na Jinsi ya Kupata Moja
  • Uaminifu ni bora kuliko Ujuzi
  • Mfano wa Maombi ya BURE
  • Kutembea kwa Maombi na Jinsi ya Kufanya
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

NEXT STEP

TII

Tumia muda wako juma hili kutii, mafunzo, na kushirikiana kulingana na ahadi ulizofanya wakati wa mazoezi ya Kundi la 3/3.

SHIRIKISHA

Omba na umuulize Mungu yule anataka ushiriki naye muundo wa Kundi 3/3 kabla kundi kukutana tena. Shiriki jina la mtu huyu na kundi kabla ya kwenda.

KIKAO KALI CHA 4

INGIA

(1 min)

Waruhusu washiriki wote na mwezeshaji waingie.

Or six.zume.training/checkin and use code: 4329

OMBA

(5 min)

Omba na kumshukuru Mungu kwa kujitolea kwa kikundi kumfuata Yesu kwa uaminifu na kumwalika Roho Mtakatifu wa Mungu kuongoza wakati wako pamoja.

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Mzunguko wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Kudumu
  • Seli za Uongozi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

READ

(5 min)

Mzunguko wa Mafundisho

Kwenye kikao hiki, tutajifunza kuhusu MFUATANO wa MAFUNDISHO ambayo huwasaidia wanafunzi kutoka kwa machache hadi mengi na kufanya umisheni kuwa harakati.

Je, umewahi kujifunza kuendesha baiskeli? Je, umewahi kufundisha mtu mwingine kuendesha? Ikiwa ni hivyo, basi kuna uwezekano unaelewa MFUATANO WA MAFUNDISHO.

Fikiria yaliyopita - kabla uendeshe baiskeli, Huenda ulimuona mtu akiendesha. Hicho ni KIELELEZO.

KIELELEZO , SAIDIA, TAZAMA na ACHA

Kielelezo ni kuonyesha mtu mwingine kama mfano jinsi inavyofanywa. Wakati mtoto anapoona mtu kwa mara ya kwanza akiendesha baiskeli, hapo wanapata wazo. Kielelezo ni vivyo hivyo - - sio eti ifanywe mara kwa mara, na klwa kawaida inastahili kufanywa mara moja.

Fikiria pale nyuma ulipoendesha baiskeli kwa mara ya kwanza. Je, ulitaka tu kuangalia? Ama ulifurahia kupanda na kujaribu? Na je, ikiwa hukupewa fursa na mtu kuendesha?

Kielelezo kingi kinaweza kuumiza mchakato. Kielelezo ni kuonyesha mtu kiasi kidogo tu - na kisha wajaribu. Ni kitu gani kilitendeka ulipojaribu mara ya kwanza? Je, walikupa tu baiskeli na wakaenda zao?

Pengine sivyo. Wakati watu wanajifunza kuendesha baiskeli, mtu huwanaye pale anapoanza kukanyaga. Akitembea kando kukusaidia kuinyosha.

Hiyo ni KUSAIDIA. KIELELEZO,SAIDIA , ANGALIA na ACHA

Kusaidia ni kumsaidia mwanafunzi kuzoesha ujuzi wake lakini hakikisha asianguke kwa nguvu. Kusaidia kunachukua muda mwingi kuliko kielelezo. Lakini sio kwa muda mrefu. Inahitaji kushikiliwa, kuelekezwa na kufundishwa, lakini ni kama kupitia pitia tu vya kimsingi. Sio kumsaidia hadi ukamilifu. Ni kuwasaidia kukanyaga.

Je, unaweza kufikia wakati mtu alikuwa anakimbia kando yako ulipoanza kukanyaga mara ya kwanza na kisha ukaongeza mwendo? Hawangelifanya hivyo kwa muda mrefu, na hungeliweza kuendesha bila kuyumba yumba.

KUSAIDIA ni kumfanya mtu kuenda na kumruhusu aende peke yake. Na anapoanza kuenda, wanakua kielelezo kwa mwanafunzi mwingine ajaye. Hata ikiwa hakuna aliyeshikilia baiskeli, haimaanishi kwamba uko peke yako. Kwa kawaida mtu mwingine huwa anakuangalia - lakini kwa umbali.

Hiyo ni KUTAZAMA. KIELELEZO, SAIDIA,ANGALIA na ACHA

Kutazama ni kumshawishi mwanafunzi hadi awe na ujuzi wake mwenyewe, hiyo yote hufanyika bila kumsaidia kuithibiti. Kuendesha baiskeli, mtu anaweza kuipanda na kuenda kwa haraka, lakini hiyo haimaanishi kwamba anaelewa sheria zote za barabarani.

Kuangalia mtu ni kuhakikisha yuko salama - hata kama hakuna mtu. Kuangalia ni kuhakikisha sio tu kwamba yule mtu anaelewa cha kufanya, na pia aifanye - hata ingawa hakuna mtu anayemwangalia.

Kwenye awamu hii ya Mfuatano wa Mafundisho, mwanafunzi atakua na akiwafundisha wengine jinsi ya kukua … kwa hivyo wafundishe wengine jinsi ya kukua.

Wanafunzi ambao wanaofanya wanafunzi wanaofanya wanafunzi wanaofanya wanafunzi. Vivyo hivyo hadi kizazi cha tatu na cha nne.

KUANGALIA ni kuhakikisha kwamba mwanafunzi anakua na sio tu kuwa nia bali pia kusaidia wengine. Kuangalia huchukua muda. Inaweza kuwa mara kumi ili mradi tu Kielelezo na Kusaidia, vikiwekwa pamoja. Inaweza kuwa muda mrefu. Lakini kusubiri kunafaa. Hatimaye - - mwendeshaji ataendesha tu baiskeli.

Hiyo ndio KUACHA kila kitu. KIELELEZO, KUSAIDIA, KUANGALI naKUACHA.

Kuacha ni kuhusu kumpa mtu umpendaye zawadi ya mwiasho-zawadi ya uhuru kuacha ni kuhusua kuandaa mtu kuenda sehemu ambayo tayari umekwisha enda lakini pia kuwapa nguvu za kuenda sehemu ambazo hawajaenda kielezo, kusaidia, kutazama na kuacha mafundisho ya mzunguko.

Kutoka kwa mmoja hadi wengi kutoka sehemu hadi kwa harakati.

JADILI

(10 min)

  1. Je, umewahi kuwa sehemu Mfuatano wa Mafundisho?
  2. Je, ulifundisha nani au nani alikufundisha?
  3. Je, mtu yuleyule anaweza kuwa sehemu tofauti za Mzunguko wa Mafunzo huku akijifunza ujuzi tofauti?
  4. Itakuaje kufundisha mtu kama huyo?

SHUGHULI

(90 min)

Kichwa: 3/3 Mkutano wa Kikundi

Changanua msimbo wa QR.

ANGALIA NYUMA - Tumia Tii, Treni na Shiriki changamoto za kipindi kilichopita ili kuingia pamoja. (dakika 30)

TAZAMA JUU - Tumia Marko 5:1-20 kama kifungu cha kusoma cha kikundi chako na ujibu maswali 1-4 katika sehemu ya Angalia. (dakika 30)

TAZAMA KWA MBELE - Tumia swali la 5, 6, na 7 katika sehemu ya Tazama Mbele ili kukuza jinsi utakavyotii, Kufunza na Kushiriki. (dakika 30)

Maudhui:

KUANGALIA NYUMA
Hatua ya 1 - Kutoa Shukrani

Chukua muda kuwa na kila mtu kushiriki kitu anachoshukuru.

Hatua ya 2 - Kushiriki Mapambano yako na Kuombeana

Acha kila mtu katika kikundi chako ashiriki kwa ufupi kitu anachopambana nacho. Acha mtu mwingine awaombee kuhusu kile wanachoshiriki.

Hatua ya 3 - Kuzingatia Kikundi

Chukua muda na ukumbuke kwa nini mko pamoja - kumpenda Mungu, kupenda wengine, kushiriki Yesu, na kuwasaidia wengine kumshiriki Yeye pia.

Hatua ya 4 - Kuingia

Acha kila mtu ajibu maswali yafuatayo:

  • Je, umetii vipi yale ambayo umejifunza hadi sasa?
  • Je, umemfundisha nani katika yale uliyojifunza?
  • Je! umeshiriki na nani hadithi yako au hadithi ya Mungu tangu tuwe pamoja kama kikundi?)

KUTAZAMA JUU

Hatua ya 1 - Alika Roho Mtakatifu wa Mungu Kuongoza

Chukua muda kidogo kuomba. Zungumza na Mungu kwa urahisi na kwa ufupi. Mwombe Roho wake Mtakatifu akufundishe kutoka katika kifungu ambacho unakaribia kusoma.

Hatua ya 2 - Soma Neno la Mungu na Uulize Maswali

Acha mtu fulani katika kikundi asome kutoka katika Biblia. Unapomaliza kusoma, kikundi kijibu maswali haya mawili:

  • Umependa nini kuhusu kifungu hiki?
  • Ni jambo gani umepata kuwa gumu au gumu kuelewa?

Soma kifungu kile kile kwa mara ya pili, na kisha kikundi kijibu maswali haya mawili:

  • Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu watu kutokana na kifungu hiki?
  • Tunaweza kujifunza nini kuhusu Mungu kutokana na kifungu hiki?

Kumbuka kushikamana na kifungu na iwe rahisi!

KUTARAJIA

Hatua ya 1 - Kuombea Kusudi la Mungu

Acha kila mtu katika kikundi chako aombe kimya na muulize Mungu maswali haya:

  • Mungu, ninawezaje kutii na kutumia yale unayonifundisha?
  • Ni nani ninaweza kufunza kutoka kwa kifungu hiki ili waweze kujifunza kutii na kukupenda Wewe zaidi?
  • Je, ungependa nishiriki ushuhuda wangu au Habari zako Njema za Yesu na nani?

Mwombe Roho Mtakatifu wa Mungu akupe majibu mahususi, majina mahususi, na hatua mahususi unazoweza kuchukua kati ya sasa na kundi lako litakapokutana tena.

Hatua ya 2 - Kukusanya Ahadi

Uliza kila mtu katika kikundi chako kushiriki kile alichosikia kutoka kwa Bwana kwa kila swali. Mtu anaweza kuwa hajasikia chochote kutoka kwa Bwana kwa swali moja, mbili, au hata zote tatu. Wanaweza tu kuripoti kwamba hawakusikia.

Lakini kumbuka, kundi linapaswa kusikia kutoka kwa Bwana. Yesu alisema, "Kondoo wangu huisikia sauti yangu." Na jinsi hatua zako za utii zinavyokuwa maalum zaidi, ndivyo itakavyokuwa rahisi kuzitii kabla hatujakutana tena.

Hatua ya 3 - Kutekeleza Mpango wako

Kabla ya kumaliza muda wako pamoja, fanya Kikundi chako cha 3/3 kigawanywe katika vikundi vidogo vya watu wawili au watatu na fanya kile ambacho umesikia Bwana akikuuliza ufanye.

JADILI

(10 min)

  1. Upenda nini hasa kuhusu kundi la 3/3? Kwa nini?
  2. Changamoto ilikuwa nini? kwa nini?

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Mzunguko wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Kudumu
  • Seli za Uongozi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

Take a Break

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Mzunguko wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Kudumu
  • Seli za Uongozi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

READ

(5 min)

Seli za Uongozi

Katika kikao hiki, tutajifunza jinsi CHEMBECHEMBE ZA UONGOZI nhuwatayarisha wafuasi kwa muda mfupi kuwa viongozi wa maisha.

Moja huwa mbili. Mbili huwa nne. Nne huwa nane. Kujizidisha moja moja. Kuongeza vizazi. Ukuaji wa kilelezo.

Huu ndio mfano Mungu aliujenga katika uumbaji wake. Hii ndio njia Mungu ananuia jamaa yake kukua. Tayari tumejifunza kuhusu mfano wa theluthi 3/3 ambao huwabaidilisha watumiaji kuwa wazalishaji, wanafunzi kwa viongozi na wanafunzi kuwa wanaowafanya- wanafunzi.

Angalia Nyuma - Angalia Juu - Angalia Mbele. Jifunze - Tii - Shirikiana.

Hii njia ya kukutana pamoja hufanya ukuaji wa kiroho unaoendelea kwa kila mmoja wa waumini na ukuaji wa uzalishaji katika kundi la wafuasi wa Yesu linaloendelea. Mfano huu huwasaidia wanafunzi kujizidisha.

Itakuaje ikiwa kundi litakuwa pamoja kwa kipindi kifupi tu, Je, bado wataweza kukua na kuzalisha Ufalme wa Mungu? Chembechembe za uongozi ni mfano wa theluthi 3/3 kazini wakati umeelewa kwamba kuna kikomo kwa wakati ambapo kundi linastahili kuwa pamoja.

Chembechembe za uongozi huandaa kila muumini kwa muda mfupi kujifunza mfano wa uzalishaji unaodumu maisha yote. Chembechembe za uongozi huwasaidia wanafunzi kuwa viongozi ambao wataanzisha makundi mapya, kufundisha makanisa mapya, na kuanzisha Chembechembe za uongozi ili kukuza jamaa ya Mungu.

Chembechembe za uongozi hufanya kazi vyema wakati kundi linasonga.

Watu wa kuhamahama, wanafunzi, wanajeshi, wafanya kazi wa ki msimu ambao wanamfuata Yesu hufanya kazi nzuri katika Chembechembe ya uongozi. Kwa sababu ya utamaduni wao, taaluma na msimu wao katika maisha - huenda wanaweza kuwa na wakati mgumu kuanzisha kundi linaloendelea, lakini wanaweza kufundishwa jinsi ya kuanzisha makundi kila mahali waendapo.

Chembechembe za uongozi pia hufanya kazi vyema wakati kundi la watu wanakuwa na imani kwa wakati moja. Jamaa, marafiki, au hata kijiji dogo chaweza kufundishwa kwa muda mfupi kuwa wazalishaji kimaisha - hata bila kufuata mtu binafsi au kufundishwa kiroho. Katika kikao cha awali, tulijifunza na kujizoesha sehemu ya mwisho ya mfano ya theluthi 3/3. Sasa tutajizoesha kwa mfano wote - sehemu zote tatu - - Angalia nyuma, angalia juu, angalia mbele.

JADILI

(10 min)

  1. Je, kuna kundi la wafuasi wa Yesu unaowajua ambao tayari wanakutana au watakuwa tayari kukutana na kuunda Kiini cha Uongozi ili kujifunza Mafunzo ya Zume?
  2. Ni kitu gani kinahitajika kuwaleta pamoja?

SHUGHULI

(90 min)

Kichwa: 3/3 Mkutano wa Kikundi

Changanua msimbo wa QR.

ANGALIA NYUMA - Tumia Tii, Treni na Shiriki changamoto za kipindi kilichopita ili kuingia pamoja. (dakika 30)

TAZAMA JUU - Tumia Matendo 2:42-47 kama kifungu cha kusoma cha kikundi chako na ujibu maswali 1- 4. (Dak 30)

TAZAMA KWA MBELE - Tumia maswali ya 5, 6, na 7 kukuza jinsi utakavyotii, Kufunza na Kushiriki. (dakika 30)

Maudhui:

KUANGALIA NYUMA
Hatua ya 1 - Kutoa Shukrani

Chukua muda kuwa na kila mtu kushiriki kitu anachoshukuru.

Hatua ya 2 - Kushiriki Mapambano yako na Kuombeana

Acha kila mtu katika kikundi chako ashiriki kwa ufupi kitu anachopambana nacho. Acha mtu mwingine awaombee kuhusu kile wanachoshiriki.

Hatua ya 3 - Kuzingatia Kikundi

Chukua muda na ukumbuke kwa nini mko pamoja - kumpenda Mungu, kupenda wengine, kushiriki Yesu, na kuwasaidia wengine kumshiriki Yeye pia.

Hatua ya 4 - Kuingia

Acha kila mtu ajibu maswali yafuatayo:

  • Je, umetii vipi yale ambayo umejifunza hadi sasa?
  • Je, umemfundisha nani katika yale uliyojifunza?
  • Je! umeshiriki na nani hadithi yako au hadithi ya Mungu tangu tuwe pamoja kama kikundi?)

KUTAZAMA JUU

Hatua ya 1 - Alika Roho Mtakatifu wa Mungu Kuongoza

Chukua muda kidogo kuomba. Zungumza na Mungu kwa urahisi na kwa ufupi. Mwombe Roho wake Mtakatifu akufundishe kutoka katika kifungu ambacho unakaribia kusoma.

Hatua ya 2 - Soma Neno la Mungu na Uulize Maswali

Acha mtu fulani katika kikundi asome kutoka katika Biblia. Unapomaliza kusoma, kikundi kijibu maswali haya mawili:

  • Umependa nini kuhusu kifungu hiki?
  • Ni jambo gani umepata kuwa gumu au gumu kuelewa?

Soma kifungu kile kile kwa mara ya pili, na kisha kikundi kijibu maswali haya mawili:

  • Je, tunaweza kujifunza nini kuhusu watu kutokana na kifungu hiki?
  • Tunaweza kujifunza nini kuhusu Mungu kutokana na kifungu hiki?

Kumbuka kushikamana na kifungu na iwe rahisi!

KUTARAJIA

Hatua ya 1 - Kuombea Kusudi la Mungu

Acha kila mtu katika kikundi chako aombe kimya na muulize Mungu maswali haya:

  • Mungu, ninawezaje kutii na kutumia yale unayonifundisha?
  • Ni nani ninaweza kufunza kutoka kwa kifungu hiki ili waweze kujifunza kutii na kukupenda Wewe zaidi?
  • Je, ungependa nishiriki ushuhuda wangu au Habari zako Njema za Yesu na nani?

Mwombe Roho Mtakatifu wa Mungu akupe majibu mahususi, majina mahususi, na hatua mahususi unazoweza kuchukua kati ya sasa na kundi lako litakapokutana tena.

Hatua ya 2 - Kukusanya Ahadi

Uliza kila mtu katika kikundi chako kushiriki kile alichosikia kutoka kwa Bwana kwa kila swali. Mtu anaweza kuwa hajasikia chochote kutoka kwa Bwana kwa swali moja, mbili, au hata zote tatu. Wanaweza tu kuripoti kwamba hawakusikia.

Lakini kumbuka, kundi linapaswa kusikia kutoka kwa Bwana. Yesu alisema, "Kondoo wangu huisikia sauti yangu." Na jinsi hatua zako za utii zinavyokuwa maalum zaidi, ndivyo itakavyokuwa rahisi kuzitii kabla hatujakutana tena.

Hatua ya 3 - Kutekeleza Mpango wako

Kabla ya kumaliza muda wako pamoja, fanya Kikundi chako cha 3/3 kigawanywe katika vikundi vidogo vya watu wawili au watatu na fanya kile ambacho umesikia Bwana akikuuliza ufanye.

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Mzunguko wa Mafunzo kwa Wanafunzi wa Kudumu
  • Seli za Uongozi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi
  • 3/3 Njia ya Mkutano wa Kikundi

KIKAO KALI CHA 5

INGIA

(1 min)

Waruhusu washiriki wote na mwezeshaji waingie.

Or six.zume.training/checkin and use code: 5451

OMBA

(5 min)

Omba na kumshukuru Mungu kwamba njia zake si njia zetu na mawazo yake si mawazo yetu. Mwombe akupe kila mshiriki wa kikundi chako mawazo ya Kristo - daima yakilenga kazi ya Baba Yake. Mwombe Roho Mtakatifu aongoze wakati wako pamoja na kukifanya kiwe kipindi bora zaidi.

ANGALIA NYUMA

(5 min)

Kabla ya kuanza, chukua muda kutazama nyuma.

Mwishoni mwa kipindi kilichopita, kila mtu katika kikundi chako alipewa changamoto ya kufanya mazoezi uliyojifunza.

Chukua muda mfupi kuona jinsi kundi lako lilivyofanya juma hili.

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Kutarajia Ukuaji usio wa kawaida
  • Njia ya Kuzidisha Matukio
  • Daima Sehemu ya Makanisa mawili
  • Uongozi Mtandaoni
  • Mafundisho ya Orodha
  • Chombo cha Sehemu nne
  • Ramani za Jenerali
  • Vikundi vya Ushauri ya Rika
  • Mpango wa miezi mitatu

READ

(5 min)

Ukuaji Usio wa Mfuatano

Katika kipindi hiki, tutajifunza jinsi ya kubomoa tabia ya kufikiria mfano duni jinsi ya kuharakisha ukuaji wa ufalme. Kuwafanya wanafuzi wanaowafanya wanafuzi kwa haraka, ni lazima tuweke maanani kwamba vitu maradufu vinaweza kufanyika kwa wakati moja na hakuna utaratibu ambapo vinaweza kufanyika.

Tunastahili kujifuza uwezo wa ukuaji USIO FUATANA. Wakati watu wanapofikiria kuhusu uzidishaji wa wanafunzi, wao hufikiria mchakato wa hatua kwa hatua.

Kwanza maombi. Kisha kujitayarisha. Kisha kushirikiana habari njema ya Mungu. Kisha kuwajenga wanafunzi. Kisha kujenga kanisa. Kisha kuendeleza viongozi. Kisha uzalishaji.

Tukijifunza kwa njia hii. Ukuaji wa ufalme unaonekana kuwa -rahisi- kufuata, mchakato wa mfuatano. Shida moja ni kwamba sio jinsi inavyofanya kazi. Shida kubwa hivyo sivyo inavyofanya kazi.

Mstari huu unawakilisha maisha ya mtu. Hapa ni kuzaliwa. Hapa ni wakati anaposikia habari njema ya Mungu. Hapa ni wakati anaamua kumfuata Yesu. Hapa ni wakati wa kwanza anashirkiana hadithi yao na hadithi ya Mungu na wanaanza kujizidisha. Na hapa ndipo maisha yao yanaishia.

(MCHORO)

Kwa hivyo ni kuanzia hapa hadi hapa - tokea wakati wa kwanza kusikia kumhusu Yesu hadi wakati wa kwanza kumshiriki Yesu ndio tunaweza kusema ni kizazi cha kiroho.

Wakati kabla ya kujizidisha. Wakati huu wote kabla jamaa ya Mungu kukua. Hivi ndivyo uanafunzi unafundishwa. Lakini tukitumia mfano kama Baraka Kuu - angalia kinachotendeka.

Wanafunzi wapya wanaanza kujizidisha mara moja. Kizazi cha kiroho kinafupishwa. Mtu anasikia habari njema ya Mungu kwa haraka. Jamaa yake Mungu inakuwa kwa haraka. Watu wengi wanaokolewa kwa uzima wa milele.

Na yote - kwa urahisi wanajizidisha wanaposonga. Na je, tukizidi kuenda? Na je, ikiwa mtu ataanza kujizidisha mapema? Na je, itakuaje wakianza kushirikiana wanaposikia mara ya kwanza kabla ya baada ya kuamini?

Wengine wako tayari kukusanya kikundi na kushirikiana yale wamesikia kutoka kwa Neno la Mungu na marafiki na jamaa kabla wamwambie Yesu "ndio". Tukionyesha hao watu jinsi ya kukusanya kundi na kushiriki walichojifunza na kuonyesha wengine nao pia wafanye hivyo, jamaa ya Mungu hukua hata haraka zaidi. Uanafuzi ni njia ya kumuendea Yesu wala sio tu kitu tunachoshirikiana baada ya wokovu.

Hii ndio njia ambayo jamaa au marafiki au hata wana kijiji wanaweza kuja kufuata Yesu. Je itakuaje ikiwa mtu ataweza kujizidisha mapema? Itakuaje ikiwa mtu ataanza kushiriki njia zake Mungu hata kabla ya kukutana na Yesu?

Wakati mwingine kundi hili huenda halina uwezo au kuwa tayari kusikiliza habari njema ya Mungu mara moja. Ila kundi hili bado linajifunza njia za Mungu- kupitia juhudi za maeandelo ya jamii au mafundisho ya uongozi.

Kundi hili lina uwezo wa kuongeza njia za Mungu- kufundisha- kutii -shirika-na kufundisha wengine kufanya. Sawa hata kabla ya kusikia mara ya kwanza kuhusu Yesu.

Hili likitokea, njia zake Mungu zimewekwa ndani ya mioyo yenye nia. Mitindo yake imesukwa ndani ya jamii na maisha ya kila mmoja. Mungu kisha tayarisha njia zake - habari njema ya Mungu itaweza kudhihirisha ukweli waliyokuwa wakipokea. Hii ndio njia taasisi, jamii, au hata nchi inaweza kuja kumfuata Yesu.

Ukuaji usiokuwa na Mfuatano bado unahitaji fikira "Iliyo Safi?" Haijalishi ni mchakato gani, swali kubwa huwa lile lile - Mchanga mzuri ni nani atakayekuwa mwaminifu? Ambaye atajifunza na kujizoesha na kushiriki njia za Mungu?

Kufichua mchanga huu mzuri - kugundua mioyo hii mizuri - inahitaji wakati wetu wote na nguvu na juhudi. Hawa ndiyo tunatoa mioyo yetu kwao. Hawa ndiyo tunatoa maisha yetu kwao. Hawa ndio wanakuza ufalme wa Mungu.

JADILI

(10 min)

  1. Ni wazo gani la kusisimua ulililosikia kwenye video hii ni lipi? Kwa nini?
  2. Wazo lenye changamoto ni lipi? Kwa nini?

READ

(5 min)

Kasi

Katika kikao hiki tutajifunza kwa nini kujizidisha kuna maana na kwa nini kujizidisha kwa haraka kunafaa asana. Kikao hiki ni kuhusu KASI. Kasi ni juu ya wakati - jinsi mambo yanafanyika pole pole au haraka. Kasi ina maana kwa sababu kule sisi sote tutakaa milele - uzima unaozidi wakati - ina idhinishwa na ule muda mfupitunaoita ""uhai".

Neno la Mungu linasema kwamba Mungu anatustahimili - hataki hata mtu mmoja apotee, bali kila mmoja ageuke na kumfuata. Mungu anatupa muda zaidi kwa sababu anajua tuko na muda mfupi kufanya yote aliyotuita kufanya na kufikia yote aliyotuita kufikia. Ili kumfuata Yesu kwa karibu, tunapaswa kufuata watu wake kwa haraka sana. Hatuwezi kupoteza muda wetu. Ni lazima tuongeze kasi.

Kanisa la kimataifa - - wafuasi wote wa Yesu, kwa pamoja - - ni kubwa kuliko ilivyokuwa. Kanisa la kimataifa - - wafuasi wote wa Yesu, kwa pamoja - - ni sehemu kubwa ya idadi ya watu duniani kuliko ilivyokuwa awali. Lakini hata na idadi hiyo kubwa - kanisa la kimataifa halikui kwa haraka kuliko idadi ya watu duniani.

Hiyo inamaanisha kwamba ingawa kunao wengi wanaomfuata Yesu kuliko hapo awali, kunao wengi ambao hamfuati Yesu na wao wote watabaki wametengwa kutoka kwake, wengi kuliko ilivyokuwa awali.
Kuwafanya wanafunzi wanajizidisha kunafaa sana. Anza na mwanafunzi. Ikiwa watajizidisha na kuwafanya wanafuzi mara moja kwa miezi 18 - mwaka moja unusu - kisha wao wanafunzi pia wafanye vivyo hivyo - kwa miaka 10, kutakuwa na wafuasi wa Yesu 64 wapya.

Watu 64 milele watakaa pamoja na Mungu mwenye upendo.

Na je, wangelienda kwa haraka kidogo? Je, wangeliongeza KASI? Ikiwa watajizidisha sasa kwa miezi 4 - robo ya mwaka - badala ya miezi 18, na hao wanafunzi pia wafanye vile - kwa miaka 10, sasa kutakuwa na wafuasi bilioni moja wapya wa Yesu.

Fikiria kuhusu hayo. Badala ya chini ya 100. Zaidi ya 1,000,000,000.

Yote kwa kuongeza KASI.

Kuenda kutoka miezi 18 hadi miezi 4 inamaanisha kwamba tunasonga kwa haraka mara - nne - unusu. Lakini kasi hiyo kila mwanafunzi aliyoitumia kwa muda wa miaka kumi inamaanisha jamaa ya Mungu inakuwa kwa haraka MARA MILIONI 15. Chini ya mia. Zaidi ya bilioni.

KASI ni muhimu

Kushiriki hadithi zetu na hadithi ya Mungu na kumuelekeza mtu kumfuata Yesu inafanya jamaa ya Mungu kukua. Kushiriki na mfuasi mpya jinsi ya kufanya vile inafanya jamaa ya Mungu kukua kama moto nyikani.
Kielelezi.

Kama chachu kwenye mkate.
Kama Zume.
Yote kwa ajili ya KASI.

JADILI

(10 min)

  1. Kwa nini ni yenye umuhimu?
  2. Unahiyaji kitu kibadilishwe katika kufikiria kwako, matendo yako, au mtazamo wako uwe bora zaidi na kipaumbele kasi kwa Mungu?
  3. Ni kitu kimoja anachoweza kufanya juma kinachoweza kuleta utofauti?

READ

(5 min)

Daima Sehemu ya Makanisa mawili

Katika kikao hiki, tutajifunza jinsi wafuasi wa Yesu wanavyoweza kuwa SEHEMU YA MAKANISA MAWILI ili kuharakisha ukuaji na kusaidia kubadilisha jamaa waaminifu wa kiroho kuwa mji unaokua - mwili pana wa waumini. Katika neno lake Mungu - tunajifunza kwamba mpango wake mkamilifu kwetu ni kuishi kama jamaa wa kiroho. Biblia inaongea kuhusu jamaa hii kama kanisa katika mambo matatu:

  • Kanisa la watu wote - mkusanyiko wa waumini ambao walikuwa, ambao ni ambao watakuwa.
  • Kanisa la kikanda au kanisa la jiji - mkusanyiko wa waumini wote katika jiji au sehemu nchi.
  • Kanisa vivi hivi - waumini wanaojikusanya katika kundi dogo kama katika jengo au kwa nyumba.

Kundi hili dogo sana - kanisa la mwanzo - ni jamaa wa kiroho wanaoishi maisha yao pamoja na hufanya kazi vyema ikiwa Jamaa inaweza kukutana na kufanya kazi pamoja kwa miezi au miaka kwa wakati.

Wakati uo huo, Yesu aliagiza wafuasi wanastahili kuwa wanaanzisha jamaa mpya za kiroho, kuwafanya wakue kama Yesu, na kuwasaidia kujifunza jinsi ya kuanzisha jamaa mpya wa kiroho, pia.

Yesu alituambia - mfanye mataifa kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, la Mwana, na la Roho Mtakatifu, na kuwafundisha yote niliyowaamuru. Sasa vitu hivi viwili vinakuja pamoja kwa njia gani - tunaweza kuwa sehemu ya kanisa na kuwa ndani ya mchakato wa kuanzisha makanisa mapya - yote kwa wakati moja?

Fikiria kanisa la kimsingi - jamaa nne tu. Kila jozi la ishara linawakilisha wanandoa wawili tofauti wanaongoza nyumba zao. Wanandoa hawa wote ni sehemu ya kanisa moja. Hivi ndivyo familia inavyoendelea. Hivi ndivyo wanaishi maisha - ndugu na dada wanaowahimiza kwa upendo na kazi nzuri.

Lakini wanandoa hawa pia wanashughulika kuanzisha jamaa mpya ya kiroho. Hawashiriki kwa njia ile wanashiriki na kundi la jamaa yao ndogo, lakini wanasaidia kuwa KILELELEZO na KUSAIDIA wakati jamaa mpya inavyoanza na kukua.

Fikiria hii - kanisa moja tu linaanziasha makanisa manne kwa wakati moja. Hivi ndivyo Mungu anaweza kufanya jamaa yake kukua kwa haraka. Hivi ndivyo kanisa linaweza kuongeza kasi yake.

Katika kikao cha awali, tulijifunza kuhusu MFUATANO WA MAFUNDISHO - KIELELEZO, KUSAIDIA, KUANGALIA na KUACHA na tunaelewa kwamba awamu hizi mbili za kwanza - KIELELEZO na KUSAIDIA zinatakikana na kupelekwa kwa haraka - ili kuwaweka wafuasi wapya wawe na afya na kuendelea kukua katika imani yao. Kwa hivyo ni kitu gani hufanyika kwa kanisa asili na makanisa manne waliyoyaanzisha? Baada ya kuwasaidia kuzindua kwa kuwa Kielelezo na Kusaidia, wanandoa hawa tayari wamesaidia makanisa haya mapya (kizazi 1) waanze kuwa kilelezo na Kusaidia, pia (kizazi 2) Kwa makanisa haya manne mapya (1 gen), wanandoa wetu (kanisa asili) kwa wakati ziko katika awamu ya KUANGALIA - kuwekea jicho maendeleo ya makanisa haya mapya (kizazi 1) na kufundisho wakiwa Kielelezo na Kusaidia makanisa mapya (kizazi 2) wanasaidia kuzianzisha wao wenyewe.

Watu wengi hawataweza kuwa kielelezo na kusaidia jamaa wa kiroho zaidi ya mara moja kwa wakati moja. Lakini wanaweza kuangalia na kufundisha makanisa kadhaa kuwasaidia kujiunganisha na mshauri wanapokua.

Hiyo inamaanisha jamaa moja wa kiroho - kundi moja dogo la kanisa - linawezakuwa sehemu ya kuzindua makundi mengine ya makanisa madogo kwa wakati ule ule. Hayo ni matunda mengi.

Kwa hivyo kitu gani hufanyika na makanisa haya yanapokuwa na yakianzisha makanisa mapya yanayoanzisha makanisa mapya? makanisa mapya? Wanabaki wakiwa wameungana kwa njia gani? Wanaishi vipi kama jamaa pana ya kiroho?

Jibu ni kwamba makanisa yote ni kama chembe katika mwili unaokua na zinaunganishwa pamoja katika mwili unaokua wavu wa mji au kanisa ki kanda. Makanisa yanahusiana. Wanashiriki DNA zao za kiroho. Wote wameunganishwa kwa jamaa ile ile ya kujizidisha ya kwanza.

Na sasa - kwa kuongozwa - wanakuja pamoja kama mwili mmoja mkubwa kufanya hata zaidi.

JADILI

(10 min)

  1. Je, ni faida gani za kudumisha jamaa ya kiroho thabiti ambayo inazaa wengine wapya ambao wanakua na kujizidisha na kuzidi badala ya kuendelea kukua na jamaa na kuitawanya ili ikue?

READ

(5 min)

Mafundisho ya Orodha

Yesu alisema -"Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake." Yesu alituambia kisha akatuonyesha tena na tena kwamba familia ya Mungu hukua vyema zaidi tunapokuwa tayari kupuuza matamanio yetu kwa ajili ya mapenzi ya Mungu.

Orodha ya Mafundisho ni zana rahisi unayoweza kutumia kusaidia kukuongoza unapowasaidia wengine kufanya sehemu tofauti za Mafundisho ya Zume kama vile Mzunguko wa Mafundisho au Orodha yao ya 100.

Je, ni stadi zipi unaona zikiimarika katika watu wengine? Ni nyanja zipi bado zinahitaji kukuzwa?

kuwa na Orodha ya Mafundisho kutakusaidia kuwa makini na kushiriki unapokuza wafuasi wa Yesu kuwa viongozi katika familia ya Mungu, kila mahali uendako.

Ndiyo, inahitaji muda na juhudi. Ndiyo, inamaanisha kujinyima na kuacha mapendeleo yetu kwa ajili ya mpango mkamilifu wa Mungu. Na ndiyo, zaidi ya hayo yote, ni jambo lenya manufaa.

Orodha ya Mafundisho ni zana rahisi kutoka Seti Yetu ya Zana ya Zume ya kukusaidia kudumu katika kazi muhimu zaidi ya maisha -- Kazi ya Mungu.

SHUGHULI

(20 min)

Coaching Checklist

JADILI

(10 min)

  1. Je, ni zana na dhana zipi ambazo unahisi utaweza kutoa mafunzo vizuri?
  2. Je, ni zana na dhana zipi unahisi ungetatizika kutoa mafunzo vizuri?
  3. Je, kuna zana au dhana zozote ambazo ungeongeza au kupunguza kutoka kwenye orodha? Kwa nini?

SHUGHULI

(5 min)

Get a Coach

Sehemu Nne na Ramani ya Kizazi ni zana iliyoundwa ili kuhudumia juhudi za harakati zinazokua.

KUMBUSHO: Makocha ya Zúme yanapatikana ili kukusaidia kutumia zana hizi katika eneo lako.

Uga

Yesu mara nyingi aliwavuta wanafunzi mbali na huduma hadi sehemu tulivu ili kuhakiki jinsi kazi ilivyokuwa ikiendelea.

Sehemu Nne hutumiwa na seli ya uongozi kutafakari juu ya jitihada za sasa na utendaji wa Ufalme unaowazunguka. Inasaidia hasa viongozi kusawazisha juhudi, ili hakuna uwanja unaopuuzwa.

Kagua slaidi mbili zinazofuata: Maelezo ya Sehemu na Mfano wa Sehemu Nne

Maelezo ya uwanja

JADILI

(10 min)

  1. Tambua uga tupu karibu nawe. Je, ni jumuiya au vikundi gani vya watu ambavyo umeunganishwa bila shughuli za injili?
  2. Ukuaji wa muda mrefu huathirije ikiwa shamba moja litapuuzwa? Toa mifano.
  3. Ni zana gani za Zúme zinaweza kusaidia katika nyanja gani?

Ramani za Jenerali

Uchoraji ramani wa vizazi (a.k.a. ramani ya kizazi au ramani ya jeni) ni zana nyingine rahisi ya kusaidia viongozi katika harakati kuelewa ukuaji unaowazunguka.

Ramani ya mti wa kizazi inaweza kuchorwa kwenye kipande cha karatasi au vipande vingi vya karatasi. Ramani hii husaidia kuonyesha mahali ambapo kuna vituo vya kuzidisha na huenda mafunzo yakahitajika. Afya ya harakati ni jambo la juu kwa viongozi na kuzaa matunda ni njia ya juu ya kupima afya.

Tazama mfano kwenye slaidi inayofuata.

JADILI

(10 min)

Tumia mfano wa Ramani ya Kizazi kujadili yafuatayo:

  1. Ni viongozi gani wanaona kuzidisha?
  2. Ni vikundi gani unatarajia kuzidisha baadaye?
  3. Ni viongozi gani wanaweza kuwasaidia na kuwaimarisha viongozi wengine?
  4. Je, unaona mtindo wa uwajibikaji dhaifu katika vizazi vyovyote?

ANGALIA

(1 min)

Dhana zilizosikika katika kikao hiki:

Zana zilizosikika katika kikao hiki:

  • Kutarajia Ukuaji usio wa kawaida
  • Njia ya Kuzidisha Matukio
  • Daima Sehemu ya Makanisa mawili
  • Uongozi Mtandaoni
  • Mafundisho ya Orodha
  • Chombo cha Sehemu nne
  • Ramani za Jenerali
  • Vikundi vya Ushauri ya Rika
  • Mpango wa miezi mitatu

NEXT STEP

TII

Jizoeze kushiriki wazo la "Pace" na rafiki na uombe kwa Bwana kuliweka kwa kina ndani ya moyo na nafsi yako. Muulize Bwana ambaye angependa umshirikishe.

SHIRIKISHA

Ikiwa tayari umeanzisha kanisa lako rahisi, shiriki dhana "Daima Sehemu ya Makanisa Mawili" na watu ndani yake. Ikiwa sivyo, shiriki na mwamini mwingine unayemjua.

Jipe moyo...

Huenda hutakuwa umejua mafundisho,ila sasa kuwa na mafundisho zaidi unapoanza makanisa ya chini na kutengeneza wanafunzi wanaongezeka kuliko wahubiri wengi na wamishonari duniani kote!

Bado Mafunzo ya Zume ni mwanzo tu! Katika kipindi hiki, tutafanya mpango wa kile kinachotokea baada ya mafunzo na tutakujulisha kwa ufupi zana utakazohitaji baadaye katika safari yako unapotekeleza yale uliyojifunza.

MAPITIO

(1 min)

Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:

Na tutaongeza zana hizi kwenye seti yetu ya zana:

  • Kutarajia Ukuaji usio wa kawaida
  • Njia ya Kuzidisha Matukio
  • Daima Sehemu ya Makanisa mawili
  • Uongozi Mtandaoni
  • Mafundisho ya Orodha
  • Chombo cha Sehemu nne
  • Ramani za Jenerali
  • Vikundi vya Ushauri ya Rika
  • Mpango wa miezi mitatu

READ

(5 min)

Uongozi Mtandaoni

Karibu tena kwenye mafunzo ya Zume. Katika kipindi hiki, tutajifunza jinsi Uongozi wa Kisheria unavyowezesha kikundi cha makanisa madogo kuongezeka na kufanya kazi pamoja, kukua viongozi wapya na kukamilisha mambo mengi mema ambayo Mungu amewapangia kwa watu wake.

Ni nini kinachotokea kwa makanisa wanapokua na kuanza makanisa mapya ambayo huanzisha makanisa mapya ambayo huanzisha makanisa mapya? Wanaendeleaje kushikamana? Je! Wanaishi maisha pamoja kama familia ya kiroho iliyopanuliwa?

Jibu ni kwamba makanisa yote rahisi ni kama seli katika mwili unaozidi na huunganisha na mtandao katika kanisa la jiji au kikanda.

Makanisa yanahusiana. Wanashiriki DNA sawa na kiroho. Wote wameunganishwa na familia ya kwanza ya kuzidisha.

Na sasa - pamoja na mwongozo fulani - wanakusanyika kama mwili mkubwa kufanya hata zaidi.

Katika ngazi ya mji na kikanda, Neno la Mungu linaonyesha kwamba mwili unaoongezeka wa waumini unatumiwa na kikundi kipya cha viongozi.

Katika Agano Jipya, kanisa linawaita watumishi hawa Wazee na Wadekani, wachungaji na waangalizi wa kundi.

Tunajifunza katika Neno la Mungu kwamba wingi wa
makanisa madogo nyumbani katika jiji la Yerusalemu, walitumikiwa na kundi la watumishi 7 - au si madekani.

Tunajifunza katika Neno la Mungu kwamba wingi wa makanisa ya nyumbani yalikuwa mji wa Efeso walitumiwa na kikundi kidogo cha Wazee - wachungaji ambao wangepaswa kufuata mfano wa Mchungaji Mzuri Yesu na kuweka maisha yao kwa ajili ya kundi lao.

Katika mji au kanda, tunaona pia kundi la zawadi tano za uongozi zinazotolewa.

Neno la Mungu linasema - Kristo mwenyewe aliwapa mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na walimu, kuwawezesha watu wake kwa kazi za huduma, ili mwili wa Kristo uweze kujengwa.

Zawadi hizi za kiroho hutolewa hivyo kikundi kidogo kinaweza kufanya kazi yote ya kanisa lakini ili waweze kutumikia na kuandaa wafuasi wa Yesu kufanya kazi - hivyo mwili wote wa waumini wanaweza kufanya kazi pamoja ili kukamilisha yote ambayo Mungu anayo katika moyo wa kufanya.

Mbali na au mahali pa kukutana na familia zao za kiroho, viongozi hawa hukutana na kuomba na kushirikiana na kuwatiana moyo kwa njia sawa sawa na kanisa lolote la nyumbani.

Mfano wa 3 / 3rds hutumiwa katika mikutano ya mafunzo ya uongozi na ushauri wa rika.

Mfumo wa Mashambani Nne hutumiwa kwa ajili ya kupanga, tathmini na kufundisha katika viwango vya juu kama ilivyo katika ngazi ya ndani.

Wakati viongozi wanapokutana wanagawana kinachotokea siyo tu kama watu binafsi lakini pia katika mtandao wao. Wao huwakilisha familia na kushiriki kuhusu ustawi wa wale wanaowahudumia.

Nafasi nzuri kwa mtandao wa familia za kiroho kwa kituo ni mahali ambapo mtandao huo unapoanza.

Mtandao wa kanisa unaotangaza kutoka Tampa utaanza kama kanisa la mji huko Tampa.

Wanapokuwa wakikua na kutumikia kote nchini, watatenda kwa niaba ya mtandao huko Florida.

Wakati wao kutuma na kutumikia kote nchini na duniani kote, wao kuanza kufanya kazi katika ngazi ya kitaifa au hata kimataifa.

Yesu alisema - Ikiwa wewe ni mwaminifu katika mambo madogo, utakuwa mwaminifu kwa watu wakuu.

Mitandao hii ya makanisa hubakia kushikamana kwa sababu ya DNA yao ya kiroho ya kiroho na mwanzo wa pamoja.

Wakati mwingine mitandao imegawanyika kwenye mitandao mingi kulingana na lugha, fursa za kukutana au sababu nyingine.

Hii ni sehemu ya ukuaji na sio tatizo.

Nia ya makanisa rahisi na wafuasi binafsi kujifunza, kutii na kushiriki Neno la Mungu ni DNA ya kiroho ya harakati. Ikiwa imepitishwa kwa mafanikio kutoka kizazi hadi kizazi, kutoka kanisa hadi
kanisa na kutoka kwa muumini hadi mwamini basi kila kitu kinachohitajika kuanzisha harakati mpya ya wanafunzi kuzidisha tayari kuna kila familia ya kiroho na kila mfuasi wa Yesu.

Wakati harakati za uzinduzi wa harakati, ndio wakati ... tunaanza kuona "chachu" inayofanya kazi kupitia unga wa jiji au hali au hata taifa. Hiyo ndivyo Ufalme wa Mungu unakuja kwa namna ambayo mapenzi ya Mungu yanafanyika duniani kama ilivyo mbinguni. Hiyo ndiyo jinsi tunaweza kumaliza Tume Kubwa kwa kufanya wanafunzi wa mataifa yote.

JADILI

(10 min)

  1. Je, kuna faida wakati mitandao ya makanisa rahisi inaunganishwa na uhusiano wa kina, wa kibinafsi? Ni mifano gani inayokuja akilini?

READ

(5 min)

Kukuza rika

Yesu alisema -"Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi."

Kikundi cha Kukuza Rika ni kikundi chenye watu wanaoongoza na kuanzisha vikundi vya 3/3. Pia kinafuata muundo wa 3/3 na ni njia yenye nguvu ya kutathmini afya ya kiroho ya kazi ya Mungu katika eneo lako.

Vikundi vya Kukuza Rika hutumia ukuzaji wa kiongozi kwa kiongozi kwa wafuasi binafsi wa Yesu, makanisa madogo, na mashirika ya huduma au hata mtandao wa kimataifa wa makanisa madogo ulionea kote ulimwenguni.

Vikundi vya Kukuza Rika hufuata mfano wa Yesu wa huduma kutoka kwenye Maandiko, huulizana maswali na kupeana maoni -- huku vikitumia mfumo wa msingi wa muda kama Kikundi cha 3/3. Lengo la vikundi hivi si kuhukumu - kumwinua mshirika mmoja na kumshusha mwingine.

Yesu alisema - "Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa."

Badala yake, lengo la Kikundi cha Kukuza Rika ni kutoa mfumo rahisi wa kuwasaidia wafuasi wa Yesu kukua kupitia maombi, utiifu, matumizi ya Neno na uwajibijaki. Kwa maneno mengine - "Kupendana."

Vinafanya kazi hivi:

TAZAMA NYUMA

Katika theluthi ya kwanza -tumieni muda katika maombi na kujaliana kama vile mngefanya katika Kikundi cha 3/3. Kisha tumieni muda kutathmini maono ya kikundi - Tunafanya vyema kiasi gani katika kudumu katika Yesu tunaposoma maandiko, kuomba, kumtumainia na kumtii Mungu, na katika mahusiano muhimu?

Hatimaye katika theluthi hii ya kwanza, acha kikundi kipitie na kujadili mipango na ahadi ambazo kila mmoja aliweka katika kipindi cha awali.

TAZAMA JUU

Theluthi ya katikati ya muda wa kikundi inatumiwa Kutazama Juu ili kupata hekima na mwongozo wa Mungu kupitia maandiko, mjadala na sala. Omba sala fupi na rahisi, ukimwomba Mungu akufundishe mapenzi yake na njia zake kupitia Neno Lake. Mwombe Roho Mtakatifu aongoze muda wenu.

Wanakikundi wanapaswa kushiriki kile walichojfunza kutoka kwa Bwana kuhusu nyanja yao ya uongozi - iwe kupitia Neno la Mungu, Sala au Wafuasi Wengine.

Ruhusu kikundi kijadili maswali rahisi yafuatayo:

  • Je, unaendeleaje katika kila sehemu ya mchoro wa Nyanja Nne?
  • Je, nini kinaendelea vizuri? Changamoto zako kubwa zaidi ni zipi?
  • Pitia ramani yako ya kizazi ya sasa.
  • Je, nini kilikupa changamoto au nini kilikuwa kigumu kwako kuelewa?
  • Je, Mungu amekuonyesha nini hivi karibuni?
  • Je, kuna maswali au maoni yoyote kutoka kwa viongozi wenye uzoefu au washirika wengine?

TAZAMA MBELE

Theluthi ya mwisho ya muda wa kikundi inatumiwa Kutazama Mbele ili kuona jinsi tunavyoweza kutumia na kutii tulichojifunza. Tumia muda kuomba kimoyomoyo na kila mwanakikundi ukimwomba Roho Mtakatifu awaonyeshe jinsi ya kujibu maswali haya:

  • Je, ni mipango au malengo gani ambayo Mungu angetaka nitekeleze kabla hatujakutana tena? (Tumia zana ya Nyanja Nne kukusaidia kumakinika katika kazi yako)
  • Je, Mshauri wangu au Wanakikundi Wengine wanaweza kunisaidiaje katika kazi hii?

Hatimaye tumieni muda kama kikundi kuzungumza na Mungu katika maombi. Ruhusu kikundi kiombe ili kila mmoja aombewe na umwombe Mungu aandaye mioyo ya wote ambao kikundi hicho kitawafikia watapokuwa wametengana.

Omba Mungu ampe kila mwanakikundi ujasiri na nguvu ya kutumia na kutii kile Mungu amemfunza katika kipindi hiki. Ikiwa kiongozi mwenye uzoefu anahitaji kumwombea kiongozi mchanga, huu ndio wakati mwafaka zaidi kwa maombi hayo.

Kwa vile vikundi hivi mara nyingi hukutana kwa mbali, kuna uwezekano mkubwa kwamba hamtaweza kushiriki Meza ya Bwana au kushiriki mlo pamoja, lakini hakikisha unatenga muda wa kuuliza kuhusu afya, familia na marafiki.

Mara kwa mara Yesu alituonyesha kwamba ingawa alitekeleza kazi muhimu zaidi, siku zote alitenga muda kwa ajili ya wale aliowapenda. Kikundi cha Kukuza Rika ni zana rahisi ya kimkakati ya kukuza viongozi bora kutoka kwenye Seti Yetu ya Zana ya Zume.

SHUGHULI

(45 min)

Kichwa: Vikundi vya Ushauri wa Rika

Maudhui:

Muundo rahisi wa kuongoza Kikundi cha Ushauri wa Rika:
ANGALIA NYUMA - 1/3 ya wakati wako

Wakati wa tatu ya kwanza - tumia muda katika maombi na utunzaji kama vile ungefanya katika Kundi la 3/3 la msingi. Kisha tumia muda kuangalia maono na uaminifu wa kikundi katika ahadi za awali: Je, unakaa vizuri kwa kiasi gani ndani ya Kristo? [Maandiko, maombi, uaminifu, utii, mahusiano muhimu?] Je, kikundi chako kilikamilisha mipango yako ya utekelezaji kutoka katika kipindi kilichopita? Zipitie.

TAZAMA JUU - 1/3 ya wakati wako

Acha kikundi kijadili maswali rahisi yafuatayo:

  • Je, unaendeleaje katika kila sehemu ya mchoro wa Nyanja Nne?
  • Ni nini kinachofanya kazi vizuri? Changamoto zako kubwa ni zipi?
  • Kagua ramani yako ya sasa ya uzalishaji.
  • Ni nini kilikupa changamoto au ni kipi ulichokiona kigumu kuelewa?
  • Mungu anakuonyesha nini hivi karibuni?
  • Je, kuna maswali yoyote kutoka kwa viongozi wenye uzoefu au washiriki wengine?

TAZAMA KWA MBELE - 1/3 ya wakati wako

Tumia muda katika maombi ya kimya na kila mtu katika kikundi akimwomba Roho Mtakatifu awaonyeshe jinsi ya kujibu maswali haya:

  • Je, ni mipango au malengo gani ambayo Mungu angetaka nitekeleze kabla ya wakati wetu ujao pamoja? [Tumia zana ya Maeneo Nne kusaidia kulenga kazi yako]
  • Je, Mshauri wangu au Wanakikundi wengine wanaweza kunisaidiaje katika kazi hii?

Hatimaye tumieni muda kama kikundi kuzungumza na Mungu katika maombi. Omba kikundi kiombe ili kila mshiriki aombewe na umwombe Mungu aandae mioyo ya wale wote ambao kikundi kitawafikia wakati wa kukaa mbali. Omba kwa Mungu kumpa kila mshiriki wa kikundi ujasiri na nguvu ya kutumia na kutii yale ambayo Mungu amewafundisha katika kipindi hiki. Ikiwa kiongozi mwenye uzoefu anahitaji kuombea kiongozi mdogo, huu ndio wakati mwafaka wa maombi hayo. Kwa kuwa vikundi hivi mara nyingi hukutana kwa mbali, huenda usiweze kusherehekea Meza ya Bwana au kushiriki mlo, lakini hakikisha kuwa umetenga muda wa kuangalia afya na familia na marafiki.

Mpango wa miezi mitatu

Katika Biblia yake, Mungu anasema, “Najua mipango niliyo nayo kwa ajili yako, mipango ya kukufanikisha na si ya kukudhuru, mipango ya kukupa tumaini na siku zijazo."

Mungu hufanya mipango, na Yeye hututarajia sisi kufanya mipango, pia.

Mpango wa Miezi Mitatu ni chombo unachoweza kutumia ili kusaidia kuelekeza umakini na juhudi zako na kuziweka sawa na vipaumbele vya Mungu vya kufanya wanafunzi wanaoongezeka.

Slaidi inayofuata itakuonyesha jinsi ya kutengeneza Mpango wako wa Miezi Mitatu. Tunapendekeza kutumia zana ya mtandaoni.

SHUGHULI

(30 min)

Three Month Plan

JADILI

(10 min)

  1. Chukua zamu kushiriki Mipango yako ya Miezi Mitatu na kila mmoja.
  2. Tafuta mshirika/washirika wa mafunzo ambaye yuko tayari kuingia nawe kila wiki. Jitolee kuwafanyia vivyo hivyo.

SHUGHULI

(0 min)

Jiunge na Jumuiya

Sehemu ya mafunzo ya Zúme inaisha, lakini mazoezi ya zana na dhana yanaendelea.

Usifanye peke yako. Tafuta jumuiya kwa ajili ya kutia moyo na kukua.

Jiunge na jumuiya ya Zume kwa kutumia msimbo wa QR.

Zúme Training — To saturate the world with multiplying disciples in our generation.