KIKAO CHA 1
INGIA
(1 min)
Waruhusu washiriki wote na mwezeshaji waingie.
Or six.zume.training/checkin and use code: 3354
OMBA
(5 min)
Anza na maombi. Ufahamu wa kiroho na mabadiliko hayawezekani bila Roho Mtakatifu. Chukua muda kama kikundi kumwalika Yeye ili akuongoze katika kipindi hiki.
MAPITIO
(1 min)
Katika somo hili, tutasikia na kujadili dhana hizi:
- Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
- Ufafanuzi rahisi wa Mwanafunzi na Kanisa
- Kupumua kwa Kiroho ni kusikia na kumtii Mungu
READ
(5 min)
Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
Karibu kwenye mafundisho ya Zume. Zume ni neno la Kigiriki linalomaanisha "chachu."
Yesu anatuambia kwamba Ufalme wa Mungu ni kama mwanamke ambaye alichukua kiasi kidogo cha " Zume" na kukiweka kwenye kiasi kikubwa cha unga uliokandwa.
Alipokuwa akichanganya, chachu ilienea hata unga wote ukachachuka.
Yesu alikuwa anatufundisha kwamba mtu wa kawaida anaweza kutumia kitu kidogo sana na kusababisha kishindo kikubwa sana!
Ndoto yetu ni kufanya yale Yesu alisema -- kuwasaidia watu wa kawaida duniani kote kutumia vifaa vidogo kutoa vishindo vikubwa katika Ufalme wa Mungu!
Maagizo ya Yesu ya mwisho kwa wanafunzi wake yalikuwa rahisi. Alisema -- Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi -enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwa batiza kwa jina la baba, na la Mwana, nala Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
Maagizo ya Yesu yalikuwa rahisi -Mkawafanye Wanafunzi
Amri yake jinsi ya kutekeleza hayo ilikuwa rahisi - mkafanye wanafunzi popote muendapo
- Mkafanye wanafunzi kwa kuwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu
- Mkawafanye wanafunzi kwa kuwafundisha yote niliyowaamuru
Kwa hivyo ni hatua zipi za kuwafanya wanafunzi?
- Tunawafanya wanafunzi kila wakati - popote tuendapo na tunapoenda
- Mtu akifanya uamuzi wa kumfuata Yesu - sharti abatizwe
- Wanapokua - tufundishe kila mwanafunzi jinsi ya kutii vitu vyote alivyoamuru Yesu.
Kwa vile kitu kimoja alichoamuru ni kufanya wanafunzi, hiyo inamaanisha kila mwanafunzi anayemfuata Yesu anastahili kujifunza jinsi ya kutengeneza wanafunzi pia.
Hao wanafunzi wanastahili kutengeneza wanafunzi. Na hao wanafunzi nao wakatengeneze wanafunzi, pia.
Kuzidisha wanafunzi. Hivyo ndivyo Zume inafanya kazi.
Ni kama chachu - ilijichanganya ndani mwa unga uliokandwa hadi wote ukawa chachu.
Wakati Yesu alipotoa amri hii ya kwenda kuwafanya wanafunzi, alitoa ahadi pia.
Yesu alisema - Nitakuwa nanyi daima. Hata ukamilifu wa dahari.
Kila mfuasi wa Yesu anapaswa kuzingatia ahadi ya kuwa Yesu yu pamoja nasi. Kwa sababu Yeye yuko!
Lakini pia inamaanisha kila mfuasi wa Yesu anapaswa kujitoa kwa ukweli kwamba Yesu anataka kila mmoja wetu atengeneneze wanafunzi. Kwa sababu Yeye alifanya.
Yesu alisema - nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye wanafunzi.
Mamlaka ambayo Yesu hutegemea wakati Anatutuma - ni mamlaka Yake
Yesu anasema hakuna mamlaka iliyo juu kuliko hiyo. Hakuna utamaduni uliyo na mamlaka zaidi.
Hakuna utamaduni uliyo na mamlaka zaidi. Hakuna sheria duniani iliyo na mamlaka zaidi.
Yesu alisema - nendeni mkawafanye wanafunzi.
Na kama Zume - chachu - tutaendelea kuenda na kukua hata kazi yote ikamilike.
JADILI
(10 min)
- Ikiwa Yesu alikusudia kila mmoja wa wafuasi Wake kutii Agizo Lake Kuu, kwa nini ni wachache sana wanaofanya wanafunzi?
READ
(5 min)
Wanafunzi na Kanisa
Karibuni tena kwenye mafundisho ya Zume.
Katika kipindi hiki, tutazungumzia kuhusu wanafunzi na kanisa.
Mwanafunzi ni nani?
Na wawezaje kumfanya mmoja? awe mwanafunzi kwa njia gani?
Je, wawezaje kumfundisha mfuasi wa Yesu kutii amri zake zote?
Je, unachukuliaje mtu ambaye aliishi maisha yake kama mtumwa wa ulimwengu na kumwezesha kuwa raia wa ufalme wa Mungu?
Maana ya neno mwanafunzi ni mfuasi.
Kwa hivyo mwanafunzi ni mfuasi wa Mungu.
Yesu alisema - Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
Kwa hivyo katika ufalme wa Mungu, Yesu ndiye Mfalme wetu.
Sisi ni raia wake, kwa mapenzi yake.
Wapenzi wake, makusudi, malengo yake, vipaumbele na maadili ni vya juu na bora zaidi.
Neno lake ni sheria. Kwa hivyo sheria ya ufalme ni nini? Je! Yesu anawaambia watu wake wakafanye nini?
Yesu alisema - Mpende Bwana Mungu kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.
Yesu alisema - Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.
Yesu alisema kwamba amri za Mungu ktika Agano la Kale - sheria zote na manabii - zinaweza kufupishwa katika mambo haya mawili - mpende Mungu na Uwapende Watu
Yesu alisema - Fanya wanafunzi
Yesu alisema - Wafundishe kutii yote niliyoamuru.
Kwa kuwa kufanya wanafunzi inajumuisha kuwafundisha yote Yesu aliyoamuru - Agano Jipya inaweza kufupishwa kwa jambo moja - Wafanye Wanafunzi
Mwanafunzi ni mfuasi wa Yesu anayempenda Mungu, anapenda watu na huwafanya wanafunzi
Basi kanisa ni nini?
Huenda huwa unafikiria kanisa ni jengo - mahali unapoenda.
Lakini Neno la Mungu linazungumzia kanisa kama mkusanyiko - watu ambao wewe umo miongoni mwao.
Neno "kanisa" linatumiwa katika Biblia kwa njia tatu tofauti:
- kanisa la ulimwengu wote - watu wote ambao walikuwa, ambao wapo na ambao daima watakuwa wafuasi wa Yesu
- kanisa la jiji au la kanda - watu wote wanaomfuata Yesu na wanaishi humo au karibu na eneo fulani la ulimwengu
- kanisa la nyumbani - watu wote wanaomfuata Yesu na hukutana pahali mmoja ama watu wengi wanapoishi.
Familia ya kiroho - wafuasi wa Yesu wanaompenda Mungu, wanawapenda watu na kuwafanya wanafunzi ambao hukutana kwenye mitaa yao ndio aina ya mwisho ya kikundi hiki cha kanisa - kanisa la nyumbani au kanisa vivi hivi.
Wakati makundi ya makanisa haya yanapokutana kufanya kitu kikubwa, kwapamoja, wanaweza kutengeza kanisa la jiji au kikanda.
Makanisa hayo yote vivi hivi yameunganishwa katika mikoa na kuenea katika historia kufanya kanisa zima.
HILO NI KANISA NA HERUFI "K" KUBWA
Makanisa yakawaida ni familia za kiroho na Yesu kama kiungo cha kati na mfalme wao.
Makanisa ya kawaida ni familia za kiroho za wanaompenda Mungu, wanawapenda wengine na wanawafanya wanafunzi ambao wanajizidisha.
Makanisa mengine yana majengo na orodha na matumizi na wafanyi kazi. Lakini makanisa yakawaida hayana haja na vitu hivi ili wampende Mungu, wapende wengine na kuwafanya wanafunzi ambao wanajizidisha idadi.
Na kwa kuwa chochote cha ziada hulifanya kanisa kuwa na ugumu kujizidisha, mafundisho yetu huacha vitu kama majengo na orodha na matumizi na wafanya kazikwa kanisa la jiji la kanda lililojengwa kutokana na uzidishaji wa makanisa yakawaida.
Kumbuka kwamba "zume" inamaanisha "chachu" -- kiumbe ambacho kinazalisha haraka haraka.
Kupitia mafundisho ya Zume - tutakuwa kama ile chachu - vivi hivi na kujizidisha.
Lakini kabla tuanze kujizidisha -tuhakikishe kwamba tunajua kile Mungu anataka kizalishwe.
Kwa sababu kuzidisha kunaweza kuwa kuzuri - lakini sio kila mara.
Saratani hujizidisha. Na inaua.
Tunawezaje kuzalisha uhai na sio kifo? Tunawezaje kuhakikisha kwamba sisi ni wanafunzi wanaoweza kuzalisha?
JADILI
(10 min)
- Unapofikiria kuhusu kanisa, kitu gani huja mawazoni?
- Kuna tofauti gani kati ya picha hiyo na kile kinachofafanuliwa kwenye video kama "Kanisa Rahisi"?
- Unafikiri ni gani ingekuwa rahisi kuzidisha na kwa nini?
READ
(5 min)
Kumsikia na Kumtii Mungu
Karibu tena kwenye mafundisho ya Zume.
Katika kipindi hiki, tutaongea kuhusu kusikia kutoka kwa Mungu na kutii yale tunayosikia.
Kupumua ni maisha.
Tunavuta hewa ndani. Tunatoa hewa nje, ni uhai.
Kupumua ni muhimu katika Ufalme wa Mungu.
Kwa kweli, Mungu anaita Roho Wake - "pumzi"
Katika Ufalme, tunapumua ndani tunaposikia kutoka kwa Mungu.
Tunapumua wakati tunasikia kutoka kwa Mungu kupitia NENO LAKE - Biblia.
Tunapumua wakati tunaposikia kutoka kwa Mungu kupitia kwa MAOMBI - mazungumzo yetu naye.
Tunapumua wakati tunasikia kutoka kwa Mungu kupitia MWILI WAKE - kanisa, wafuasi wengine wa Yesu.
Tunapumua tunaposikia kutoka kwa Mungu kwa njia ya kazi zake - matukio, uzoefu na wakati mwingine hata mateso na kuteseka ambapo anaruhusu watoto wake kupitia.
Katika Ufalme tunapumua NJE tunapotenda kwa ajili ya yale tunasikia kutoka kwa Mungu. Tunapumua NJE wakati TUNATII.
Wakati mwingine kupumua nje kwa KUTII inamaanisha kubadilisha mawazo yetu, maneno yetu au matendo yetu ili kuwaleta pamoja na Yesu na mapenzi Yake.
Wakati mwingine kupumua kwa KUTII kunamaanisha kugawana kile Yesu ameshiriki nasi - kupeana kile alichotupa - ili wengine waweze kubarikiwa kama vile Mungu anavyotubariki.
Kwa mfuasi wa Yesu - hii kupumua NDANI na kupumua NJE ni muhimu. Ni maisha yetu.
Yesu alisema - Mwana hawezi kufanya kitu peke yake. Anafanya tu yale anayoyaona Baba akifanya. Chochote Baba anachofanya, Mwana pia hufanya.
Yesu alisema - Sineni kwa mamlaka yangu mwenyewe. Baba aliyenituma ameniamrisha cha kusema na jinsi ya kusema.
Yesu alisema kwamba kila neno alilosema na kila kazi aliyotimiza ilitokana na KUSIKIA kutoka kwa Mungu na KUTII yale aliyasikia.
Pumua NDANI - Sikia kutoka kwa Mungu.
Pumua NJE - Tii yale unayosikia na ushiriki na wengine.
Yesu alisema kwamba wafuasi wake pia watasikia kutoka kwa Mungu kwa sababu ya Roho Mtakatifu wake - Kupumua Kwake - ambayo itapumuliwa ndani ya kila mmoja wetu anayemfuata.
Yesu alisema - Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha vitu vyote na kuwakumbusheni kila kitu nilichowaambia.
Kupumua NDANI- Sikia kutoka kwa Mungu.
Pumua NJE- Tii yale unayoyasikia na uishiriki na wengine.
Yesu alikuwa anatuonyesha jinsi ya kuishi.
Kwa hivyo tunaisikiaje sauti ya Mungu? Tunajuaje nini cha kutii?
Yesu alijiita mwenyewe "Mchungaji Mzuri". Yesu aliwaita wafuasi "kondoo"wake.
Yesu akasema - Kondoo wangu husikia sauti Yangu, na ninawajua, na wananifuata.
Yesu alisema - Yeyote aliye wa Mungu husikia kile ambacho Mungu anasema. Sababu hamsikii ni kwamba ninyi si wa Mungu.
Kama wafuasi wa Yesu, tunapaswa kujitolea kusikia sauti Yake.
- TUNASIKIA sauti yake kwa kuwa kimya.
- TUNASIKIA sauti yake kwa kumzingatia Yesu.
- TUNASIKIA sauti yake katika mawazo yetu, maono yetu, hisia zetu na dhana zetu.
- TUNASIKIA sauti yake tunapoandika na kuhakiki kile tunachosikia.
Si kila sauti, sio kila wazo, sio maono, hisia au dhana ni sauti ya Mungu.
Wakati mwingine ni sauti ya adui
Yesu alisema adui yetu ni mwongo na baba wa uongo. Yesu alisema adui yetu huja kuiba, kuua na kuharibu.
Lakini Mungu anasema kwamba TUTASIKIA kutoka kwake na tutajua ni Yeye wakati anapozungumza
Kwa kujizoeza na maombi, tunaweza kujua sauti ya Mungu vyema. Tunaweza kujifunza kujua kama tunachosikia ni kutoka kwa Mungu au sauti nyingine.
Hapa kuna njia ya kujaribu yale tunayosikia:
- Wakati Yesu anapoongea - sauti yake itakuwa thabiti Neno lake Lililoandikwa -
- Biblia - tayari imetueleza. Sauti yake haitakinzana na sauti ilioandikwa.
- Wakati Yesu anapoongea - sauti yake itaipa mioyo yetu hisia ya tumaini na amani. Sauti yake haitatuacha ama kutuvunja mioyo. Yesu hahukumu. Yesu hurekebisha kwa upendo.
- Sauti ya Yesu haitaelezea matendo ya mwili - uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu na uchawi, uadai, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, mambo haya sio sauti ya Mungu.
- Wakati Yesu anapoongea - sauti yake itatuonyesha matunda ya Roho wa Mungu - upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.
Wakati Yesu akisema - Sauti yake hutupa hisia za kujiamini badala ya wasiwasi. Tunapata ndani mwetu ujuzi na amani kwamba kile tunachosikia kinatoka kwa Mungu. Hatuwezi kusikia kila kitu mara moja. Tunaweza kusikia sehemu tu ya kile tunachohitajika kujua. Lakini kile tunasikia itakuwa imara - si ya kuhama hama au kujibadilisha.
Habari njema kwa kila mfuasi wa Yesu ni kwamba tunapopumua NDANI na KUSIKIA kutoka kwa Mungu na tunapopumua NJE na KUTII tunachosikia na kushirikiana na wengine tulichosikia - Mungu ataongea wazi wazi.
Pumzi yake itapumua kupitia sisi hata zaidi.
TUTASIKIA sauti yake wazi zaidi.
TUTAJUA sauti yake na sio nyingine.
TUTAONA kazi ndani yake duniani na kujiunga naye kufanya kazi pamoja
Tunapumua. Tunapumua nje. Uzima.
JADILI
(10 min)
- Kwa nini ni muhimu kujifunza na kusikia na kutambua sauti ya Mungu?
- Je, kusikia na kumuitikia Bwana ni kama kupumua? Kwa nini au kwa nini sivyo?
ANGALIA
(1 min)
Dhana zilizosikika katika kikao hiki:
- Mungu Anatumia Watu wa Kawaida
- Ufafanuzi rahisi wa Mwanafunzi na Kanisa
- Kupumua kwa Kiroho ni kusikia na kumtii Mungu
NEXT STEP
TII
Jizoeze kushiriki ufafanuzi huu na rafiki na uombe kwa Bwana aziweke kwa kina ndani ya moyo wako na nafsi yako. Muulize Bwana ambaye angependa uwashiriki.
SHIRIKISHA
Shiriki ufafanuzi na yeyote ambaye Bwana anakuvutia kufanya hivyo naye. Kisha wape vifaa ili kushiriki na mtu mwingine.
