concept

Mungu Anatumia Watu wa Kawaida

Shiriki ukurasa huu

Je, umewahi kujiuliza kanisa lilianza vipi? Hapo mwanzo hakuna aliyekuwa mtaalamu. Umeshangaa? Jambo jema ni kwamba Mungu alikuwa na mpango ambao haukuhitaji wataalamu. Mungu hutumia watu wa kawaida. Alifanya hivyo kuanzisha vuguvugu la kwanza la kanisa. Naye anafanya hivyo leo. Kanisa la kwanza liliwatuma watu wa kawaida kote ulimwenguni kuwaambia wengine kuhusu Yesu. Liliwatuma watu wa kawaida kusimama mbele ya magavana na majenerali na watawala na wafalme. Liliwatuma watu wa kawaida kuponya wagonjwa, kuwalisha wenye njaa, kufufua wafu, na kuwafundisha watu wote ulimwenguni amri zote za Mungu. Kanisa la kwanza liliwatuma watu wa kawaida kuubadilisha ulimwengu. Nao waliufanya.

Ndoto yetu ni kufanya kile Yesu alisema -- kuwasaidia watu wa kawaida duniani kote kutumia zana ndogo kuleta athari kubwa katika Ufalme wa Mungu! Maagizo ya mwisho ya Yesu kwa wafuasi Wake yalikuwa rahisi. Alisema — Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Kwa hivyo nendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kutii yote niliyowaamuru. Nami nitakuwa pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Amri ya Yesu ilikuwa rahisi - fanyeni wanafunzi.

Maagizo yake kuhusu jinsi ya kufanya hivyo yalikuwa rahisi:

  • Fanyeni wanafunzi popote mnapokwenda;
  • Fanyeni wanafunzi kwa kuwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
  • Fanyeni wanafunzi kwa kuwafundisha kutii yote aliyoyaamuru.

Basi ni hatua zipi za kufanya mwanafunzi?

  • Tunafanya wanafunzi wakati wote - popote tunapokwenda na tunapoendelea kwenda.
  • Mtu anapoamua kumfuata Yesu - anapaswa kubatizwa.
  • Kadiri wanavyokua - tunapaswa kumfundisha kila mwanafunzi jinsi ya kutii kila kitu ambacho Yesu aliamuru.

Kwa kuwa mojawapo ya mambo aliyoyaamuru ni kufanya wanafunzi, hilo linamaanisha kwamba kila mwanafunzi anayemfuata Yesu anahitaji kujifunza jinsi ya kufanya wanafunzi pia.

Jiulize

  • Ikiwa Yesu alikusudia kila mmoja wa wafuasi Wake kutii Agizo Lake Kuu, kwa nini ni wachache sana wanaofanya wanafunzi?
    • Je, wazo kwamba Mungu hutumia watu wa kawaida ni tofauti na kile ulichokuwa umejifunza au kudhani kuwa ndiyo mpango?

Anza Zúme Training leo

Ni bure kabisa, na unaweza kuanza wakati wowote—endelea kwa kasi yako mwenyewe, popote ulipo.

Jisajili Bure